Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
Mwanamuziki wa Uingereza na aliyewahi kushiriki Britain’s Got Talent, Natalie Okri, amezua gumzo baada ya kudai kuwa baadhi ya wigs za nywele halisi huleta mikosi na bahati mbaya.
Katika video aliyopost Instagram, Natalie alisema:
• Nywele halisi zinabeba utambulisho wa mtu, zina DNA (vinasaba) ambayo haifanani na mtu yoyote yule Duniani. Unapovaa wigi la Nywele ya mtu unabeba utambulisho wa mtu mwingine.
Wigs nyingi hutengenezwa hutoka ASIA ambapo sababu ya kufanya huwa hizi;-
1) WANAWAKE hutoa kama sadaka kwenye baadhi ya mahekalu Asia kutokana na dini au imani zao, ambapo wanawake hao huamini wakinyolewa Nywele zote wataondoa mikosi na kuanza upya, wataondoa umasikini na matatizo.
2) Watoto wadogo (pia WATU wazima) hulazimika kukatwa Nywele na wazazi wao Kwa sababu za kiuchumi pengine Bila ridhaa zao
Baada ya hapo, nywele hizo hukusanywa au huuzwa kwa mawakala mbalimbali pia kupitia majukwaa kama AliExpress na Alibaba.
Anadai wanawake wa Kiafrika hununua wigs hizo bila kujua kwamba zinaweza kubeba mizigo ya kiroho au mikosi ya wenyewe.
Natalie alisisitiza kuwa yeye kama Mkristo, na anaona nywele hizo zinapingana na imani yake kwa sababu zinahusishwa na miungu au nguvu zisizojulikana na watu hao mara nyingi huabudu Miungu.
🗣️Anasema "Tunavaa wigs zinazotoka kwa mtu aliyenyoa nywele zake ili aondokane na mikosi yake. Hatutambui kwamba tunabeba mizigo yao vichwani mwetu."
Natalie Okri alipata umaarufu mwaka 2009 kwenye Britain’s Got Talent, na sasa anaonekana kutumia jukwaa lake kuzungumzia imani na mitazamo ya kiroho kuhusu urembo.
............................................................