Wiki iliyopita nimekutana na jamaa aliyenibugudhi gheto kwa sababu ya kuchoma udi

Nipo serous kaka nahitaji kuelimika. Sema dogo anahisi nina kejeli imani yake . Siwezi vuka mpaka huo
Nimeelezea pia ktk comment yangu. Ubani unatajwa sana katika maandiko. Zamani nilikua nikiamini haya ni mambo ya kishirikina. Lakini nikaja pewa Elimu na viongozi wa kanisani vzr tu juu ya ubani. Na akanieleze ubani unavyotengemezwa kwa ile miti ya matawi. Hata mtoto Yesu alipozaliwa walimpelekea zawadi ya ubani, manemane na pesa. That means haikua kitu kibaya. Sisi wakatoliki ubani hutumika sana kanisani katika adhimisho la misa takatifu ya Ekaristi takatifu. Hutumika kupatakatifusha na kufungua anga kwaajili ya kupeleka maombi yako. Nikuambie tu, haya maombi huwa ni mazito mno. Na huwa nafanya nadra sana. Na huwa nayafanya pale napokosewa kwa mambo ya msingi. Nimewahi fanya mara 3 na nikajibiwa exactly. Kuna majirani zangu tunasali nao jumuiya walinishangaaga sana wakanambia hujua unajua hili? Ilikua mwaka jana mwishoni. Mwaka huu ndo nilisali juu ya mambo kadhaa. So ni imani hasaaa..

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Maelezo yako yamejirudia . Nachotaka kufahamu ni mambo 3

1: Ubani ni nini? (Ni magome ya miti na ni mti gani/ ni matunda / ni mizizi nk..)

2: Kuna mahusiano gani kati ya ubani na maombi/dua.? (Mana kama ni moshi je tukichoma mti mwingine wowote wenye moshi ni sawa? Na je ni kiomba bila ubani dua inapungua uzito na kwanini)?

3: Mungu anavutiwa na nini kwenye ubani? Harufu , Moshi au rangi hadi akubari kwa haraka dua inayoombwa kupitia Ubani kuliko dua zingine?.. (Mana unauchoma ndani afu una niambia unasafisha anga kivipi? Wakati ule moshi hata ozone ya kwanza haufiki na kama ni harufu hata nje haifiki.?)
 
Ukisoma Kwenye Biblia Mungu alikuwa anavutiwa sana na Sadaka za Kuteketezwa . Maana Yake Sadaka Zilichomwa Moto na Moshi ukapanda Juu. Na Kuna Sehemu Alisema Kabisa Kwamba Anavutiwa na Moshi utokao Kwenye Sadaka Hizo

Kumbuka Miti aliyoiumba Mungu Ni Dawa Ya Vitu Vingi sana. Tatizo sisi Tumeacha Asili Yetu. Miti Inatumika Kuponya,Kufukuza Roho mbaya,Kujitakasa n.k n.k Na Ipo ya Aina Mbalimbali kwahiyo hata Ubani Ni Moja Wapo
 
Sisi tunaongelea imani kumbe wewe unaongelea sayansi mkuu? Sasa ubani kumbe unajua kabisa umetokana na magome ya miti swali lako ni lipi hapo? Umejitahidi sana kuweka swali lako kitaalam lisionekane ni kejeli ila i read u.
Jioni njema

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Ko Ubani unatumika kama Sadaka ? Na je tukichukua mazao, mifugo au pesa tukachoma moto na kufanya maombi mungu anapendezwa nazo?
 
Jukumu la mtu mwenye mwenye imani ni kumuelimisha asie na imani ili aamini kama yeye. Sasa mnatakiwa kutuelimisha kunako ubani ili nasisi tuanze kuuwasha mana tuna mashida kibao Mungu anajifanya hatuoni kumbe kuna njia rahisi yakumfanya mungu atuelewe
 
Je kwa Imani yako wewe mkuu huyo NENO ni NANI?
 
Nahisi Bado Hujanitambua. Na Haupo Serious Kuelimika, Siku Ukiwa Tayari Utatafuta Elimu Kwa U serious
Ndio sijakuelewa na ndo mana naendelea kukusumbua ili nitoke na kitu. Sipo hapa kurumbana. Nachotaka kufaham ni nguvu ya ubani Kwenye maombi ili ikiwezekana nianze kutumia. Au nije pm nn?
 
Uko ulivyo kwa vile unachoma sana uvumba au Mwenyezi Mungu anabariki juhudi zako za kufanya kazi na zinazaa matunda ya kutosha? Aliyekupa wewe jana ndiye atakayempa yule kesho, heshimu watu ndugu yangu, kesho ina siri kubwa.
 
Usimshangae jifunze kunyamaza na kusamehe yasije yakageuka kwako hakuna anae jua kesho eeee,huenda nae atakushangaaaa
 
Sijaelewa kabisa kosa la huyo mtu mpaka akawa masikini kama unavyomsema?

Kawa masikini kisa hachomi huo ubani wako? Kawa masikini kisa kukupinga ulipokuwa unachoma ubani? Kuna uhusiano gani kati ya ubani na imani yako kwa huyo mtu?

Unachotakiwa kufahamu

1. Si kila mtu lazima awe mkristo au muislamu! Hapa tupo wasio na dini, wenye dini tofauti na hizo mbili

2. Kuna watu wakinusa halufu ya manukato yoyote wana allerge nayo! Mfano Mimi parfume kidogo tu nikinusa napata kizunguzungu
 
K
Kaka wanasaikolojia tumeshakujua wewe ni mtu wa mrengo gani!!!!Unajitahidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…