Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Ni zaidi ya Wiki moja sasa tangu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, alipotoa agizo kwa Jeshi la Polisi kuwasaka na kuwachukulia hatua wale waliohusika katika wizi wa vitabu vya majina ya wakazi katika kituo cha Josho, kijiji cha Kikelelwa, wilayani Rombo. Tangu wakati huo, hakuna taarifa za hatua zilizofikiwa, hasa ikizingatiwa kuwa agizo hilo lilijiri kufuatia wizi wa vitabu viwili vilivyokuwa na majina ya wananchi 1,105.
Nakumbuka polisi waliripoti kuwashikilia watu wanne kwa mahojiano kufuatia na tukio hilo. Hata hivyo, taarifa rasmi kuhusu uchunguzi huo bado hazijatolewa kwa umma.
Soma: Kilimanjaro: Wasiojulikana waiba madaftari ya kujiandikishia, wengine wachoma moto Ofisi ya Mtendaji
Soma: Kilimanjaro: Wasiojulikana waiba madaftari ya kujiandikishia, wengine wachoma moto Ofisi ya Mtendaji