Mohammed Hamad
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 3,988
- 1,308
Kila mwanamke ameumbwa na hulka ya kuamini kuwa anasifa ya uzuri. Hivyo basi wanawake tunaamini kwamba uzuri huo unaonenaka kwa nje kupitia mivuto.
Mivuto hiyo huwavuta wanaume wengine wakusalimie, wengine wapige jicho ili mradi wajiburudishe, na wale walio na ushujaa na ujasiri huwa hawasiti kukutongoza, na hapa kila mwanaume ana gia zake za kumwingia mwanamke.
Je dada mwenzangu huwa unajisikiaje ikipita wiki nzima hujasalimiwa na wavulana wenye jicho la kukutamani, hujatongozwa na wala hujasifiwa?
Binafsi last week ndio ilikuwa wiki niliyokuwa nimekosa kabisa watu wa kunichangamkia, nkajiuliza sana je nimezeeka au nyota yangu imetembelewa na mtu (lm kidding, siamini mambo ya nyota)
Je wanaokutongoza kwa wiki wangapi? na unawakubalia wangapi?
Asante.