Wiki ya 41 sasa mtoto hajazaliwa

Wiki ya 41 sasa mtoto hajazaliwa

chichimizi

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2015
Posts
1,074
Reaction score
339
Habarini wadau

Mke wangu ana ujauzito na tarehe ya matarajio ilikua ni tarehe 1 lakini naona siku zinaenda tu mtoto wangu hazaliwi kazi yake ni kurukaruka tu tumboni kwa mama yake.

Je watalamu hapa shida iko wapi?
 
Kawaida tu mkuu wala usipate hofu. 'matarajio' mara nyingine huwa wanakosea ku-approximate. Ongeza wiki moja mbele, mwambie mamaa aongeze mazoezi na pia nlisikia juisi ya mananasi inasaidia kuongeza uchungu.
Mama yangu aliniambiaga ujauzito wa kunizaa mimi aliubeba kwa miezi 12, imagine subira kiasi ilihitajika katika mtihani wake.
 
Tena ondoa hofu, tarehe 1 na leo ndio kwanza tarehe 7. Wife alipitisha wiki kadhaa na alijifungua salama. Msingi asilale kila wakati, afanye mazoezi, unaweza kumchukua mkatembea kilometa moja pole pole tu mkarudi
 
Kawaida tu mkuu wala usipate hofu. 'matarajio' mara nyingine huwa wanakosea ku-approximate. Ongeza wiki moja mbele, mwambie mamaa aongeze mazoezi na pia nlisikia juisi ya mananasi inasaidia kuongeza uchungu.
Mama yangu aliniambiaga ujauzito wa kunizaa mimi aliubeba kwa miezi 12, imagine subira kiasi ilihitajika katika mtihani wake.
Miezi 12 unamaanisha mwaka mmoja!!!
Utani huo
 
Habarini wadau jamani mke wangu anaujauzito na tarehe ya matarajio ilikua ni tarehe 1 lakini naona siku zinaenda tu mtoto wangu hazaliwi kazi yake nikurukaruka tu tumboni kwa mama yake.
Je watalamu hapa shida iko wapi?
Hospital wamesemaje??
 
Hospital nimeenda nimeambiwa nitulie soon itakua Poa tu.

Lakini naona kama sio kweli hivi maana kesho linaanza wiki la 42 aiseee nadata kabisa
 
Hospital nimeenda nimeambiwa nitulie soon itakua Poa tu.

Lakini naona kama sio kweli hivi maana kesho linaanza wiki la 42 aiseee nadata kabisa
Kuwa na amani baba kijacho, ni kawaida
upload_2018-1-7_7-27-24.png
 
Aiseee maana kuna clip nilichek YouTube inadai week 42 na kuendelea ile umbricocod inastop functioning nikaonaeeeee isewe nongwa nikapata mawazo ya kwenda kupiga kisu
 
Kawaida tu mkuu wala usipate hofu. 'matarajio' mara nyingine huwa wanakosea ku-approximate. Ongeza wiki moja mbele, mwambie mamaa aongeze mazoezi na pia nlisikia juisi ya mananasi inasaidia kuongeza uchungu.
Mama yangu aliniambiaga ujauzito wa kunizaa mimi aliubeba kwa miezi 12, imagine subira kiasi ilihitajika katika mtihani wake.
Acha kupotosha
 
Wiki ya 42 huwa ni ya mwisho ya matazamio baada ya hapo daktari ataamua hatua ya kuchukua ila na ultra sound iwe inaendana na hayo mahesabu yako.
 
Mimba ikipitiliza miezi 11 ndo huwa wanafanya operation maana anakuwa amekuwa mkubwa sana na mifupa ya fuvu imekomaa hivyo hawezi kupita kwa njia ya kawaida. Ila wiki ya 41 ni kawaida mkuu
 
Wiki ya makisio ya mtoto kuzaliwa ni wiki ya 40. Endapo amepitiliza wiki mpaka wiki ya 41 mpeleke hospitali wakafanye induction of Labour. Watamuwekea vidonge vya uchungu. Kuchelewa zaidi ni kutafuta matatizo

Ova
Heeee sasa mbona tena mnanitisha?

Lipi jemaaa?
 
hospital nako kuna majanga yake isije ikawa ulikutana na Dr mwenye stress zake akakujibu simple tafuteni 2nd opinion
 
Back
Top Bottom