Wiki ya huduma kwa mteja: Vitu gani unapenda ufanyiwe na Watoa Huduma?

Wiki ya huduma kwa mteja: Vitu gani unapenda ufanyiwe na Watoa Huduma?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Wakuu,

Nimeona taasisi na ofisi mbalimbali wanaadhimisha Wiki ya Huduma kwa Mteja ambayo imeanza Oktoba 5 hadi 9, 2026. Lakini kwangu mimi, kama mnufaika wa huduma, kuna vitu au tabia ambazo huwa sipendi kufanyiwa na watoa huduma.

Moja wapo ni pale ninapofika sehemu, kama dukani, kisha mtoa huduma anaacha kunihudumia na kwenda kumhudumia mteja mwingine kwa sababu tu ni rafiki yake au wanafahamiana. Kwa kweli, hii huwa naiona kama dharau kwa mteja.

Tabia nyingine ni hii ya kukuta mtoa huduma anachati au anaperuzi mtandaoni, na baada ya kufika unakuta hana habari na wewe. Yaani huwa nashindwa kuelewa kama hawa jamaa huwa wanajali huduma wanazotoa.

Haya na wewe, Mwana Jukwaa, ni vitu gani hupendi kufanyiwa na watoa huduma?
 
Kusikilizwa
Kujaliwa
Kupewa huduma kwa wakati
 
Back
Top Bottom