Wiki ya Maji bila maji kwenye maeneo mengi, serikali mmeamua kutung'ong'a wananchi! Matamko elfu huku huduma ikiwa sifuri!

Wiki ya Maji bila maji kwenye maeneo mengi, serikali mmeamua kutung'ong'a wananchi! Matamko elfu huku huduma ikiwa sifuri!

Precious Diamond

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
753
Reaction score
1,699
Wakuu,

Hamuoni kama inachekesha, yaani kama vile serikali na wizara ya maji inatung'onga! Tunalalamika ukosefu wa huduma hii kila leo, kwa wiki tunapata maji mara moja halafu huko kwenye majukwaa wanajitapa kuna maji ya kutosha!

Maji yapi? Haya ya kutosha kwenye kisoda tunayogombania kila leo. Ilikuwa hukutani na wauza maji lately lakini sasa hili limerudi kwa kasi!

Kitu ambacho kinanifikirisha ni kwanini karibu na uchaguzi huduma hizi zinakuwa kwenye upungufu mkubwa, ni sawa hata kwenye umeme, halafu ghafla unaona uuzaji wa majenereta unaongezeka, maboza nayo yanataradadi mtaani,, yaani ni kama ka project ka kukusanya hela zaidi kwa wananchi na maigizo ya kutengeneza tatizo ili waje kulitatua na kupewa sifa.

Inabidi mjisikie aibu kwa huu upuuzi mnatufanyia wananchi Wizara ya Maji
 
Huku kwetu ni kilio

kilio.jpg
 
Back
Top Bottom