Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko anawakaribisha Wabunge na Wananchi katika Wiki ya Nishati itakayofanyika katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma tarehe 15, Aprili 2024 hadi tarehe 19 Aprili 2024.
Hii ni fursa kwa Wabunge na Wananchi kufahamu utekelezaji wa Sera ya Nishati katika mwaka 2023/2024 na uelekeo wa Sekta ya Nishati katika mwaka 2024/2025 ili kukuza uchumi wa Nchi.