Wiki ya siku 4 kikazi imefanyiwa majaribio UK. Je, tutafuata mkumbo na jee inatufaa?

Wiki ya siku 4 kikazi imefanyiwa majaribio UK. Je, tutafuata mkumbo na jee inatufaa?

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Makampuni kadhaa yametoa matokea chanya kuhusu kuwa na siku nne tu za kazi kwa wiki.

Utafiti huo ulioonza mwaka 2022 umeshaanza kushirikisha na makampuni ya nchi nyengine nje ya Uiengereza.

Cha kujiuliza ni jee watanzania na waafrika kwa ujumla wiki hii itawafaa na jee watafuata mkumbo kama ambavyo kinachoanzia huko lazima kifikishwe na huku.

The four-day work week is here to stay at UK companies that tried it

Hakuna haja ya kumuhenyesha binadamu.Nfiyo maana tunakufa mapema.Siku nne zinatosha kwa wiki.
 
Kuna sehemu na sehemu.

Mfano. Mwalimu kwa wiki yuko na vipindi siku 4. Analazimika kukaa ofisini masaa 8 ya siku ya 5 kwa sababu gani?

Ni kweli yupo kazini. Lkn Time value ya kazi anayo ifanya haviendani.
 
Hakuna haja ya kumuhenyesha binadamu.Nfiyo maana tunakufa mapema.Siku nne zinatosha kwa wiki.
babu zenu walifanya kaz siku nne ili nyie muje kuish kifahari leo hii?
 
Whatever mkuu, yan ambavyo tuna shida ya vyoo, Visima, mara umeme, mara madarasa, yan tuna mashida kibao, halafu tufanye kazi siku 4 ? Hizo shida atasolve nani?
maskin huwa wavivu
 
Kwa huku kwetu tunahitaji siku 6 kwa wafanya kazi na siku 4 za masomo na siku 1 ya stadi za kazi kwa watoto wanaosoma. Twende na mwendo wetu wala tusiwaige hao magasho tutafika tu mdogo mdogo.
 
Kwa huku kwetu labda itokee tu lakini hizi kampuni usipoenda kazini unaumwa unakatwa mshahara waje wakwambie ufanye siku 4 sioni kabisa
 
Australia pia wako mbioni.

Sisi huku kwetu uchumi utaanguka kabisa maana sasa unachechemea.
 
Hoja sio kuwa Nyuma, hii inatokana na ukuajiaji wa technolojia hasa upande wa matumizi ya AI.
Hii AI nayo ni utumbo tu.
haina lolote la maana.Hakuna kitakachofanyika kwa ufanisi bila akili halisi ya binadamu.
Kuna maendeleo hutangazwa sana na baadae yakaonekana ni ulimbuke tu.Mfano gari za umeme na zile za kujiendesha wenyewe bila dereva.
 
Makampuni kadhaa yametoa matokea chanya kuhusu kuwa na siku nne tu za kazi kwa wiki.

Utafiti huo ulioonza mwaka 2022 umeshaanza kushirikisha na makampuni ya nchi nyengine nje ya Uiengereza.

Cha kujiuliza ni jee watanzania na waafrika kwa ujumla wiki hii itawafaa na jee watafuata mkumbo kama ambavyo kinachoanzia huko lazima kifikishwe na huku.

The four-day work week is here to stay at UK companies that tried it

Week end ianze ijumaa,au Kama vipi j2 itolewe tubaki na ijumaa na jmos
 
Hizo kazi zenyewe zipo wapi ? Watu wanatafuta kazi hata siku moja kwa wiki (Kibarua wanakosa) !!

Issue ni kwamba watu hawana ajira zenye ujira na wale watumishi wa UMMA sababu kazi hazipo na wengi wanazitaka wafanye kazi kabisa siku sita na ile ya saba wapeane zamu za kuhakikisha huduma inapatikana 24/7 (kama inahitajika)
 
Back
Top Bottom