Wiki ya Usalama Barabarani: Polisi na Serikali mmeshindwa vibaya kudhibiti bajajI na bodaboda?

Wiki ya Usalama Barabarani: Polisi na Serikali mmeshindwa vibaya kudhibiti bajajI na bodaboda?

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16,419
Reaction score
26,594
Polisi wanatamba kuwa kutotii sheria utakamatwa na utachukuliwa hatua za kisheria.

Kuna kundi kubwa la watumiaji wa barabara wanamiliki bajaj na bodaboda nchini, kundi hili liko juu ya sheria.
HAKUNA wanaolidhibiti kundi hili, si polisi au chombo chochote cha dola.

Na kundi hili kwa kiasi kikubwa ni kero:
  • Kuna ajali za barabarani
  • Kuna kubebana mishkaki
  • Kuna kutotii alama na taa za barabarani
  • Kuna wanasiasa wanawatumia bodaboda kama msingi wao wa kisiasa.
  • Bodaboda na hata bajaji wengine hawana leseni kabisaa
Bado serikali inaendelea kusajili vyombo hivi utafikiri hakuna tatizo.

Hivyo basi kauli mbiu ya Polisi ambao ni wasimamiaji wa sheria za barabarani inakuwa haina maana kabisa.
Na kwa mlolongo wa matatizo niliyoorodhesha, serikali yenyewe na wanasiasa wanahujumu usalama barabarani.

Na hili la eti Wiki ya Usalama barabarani linakosa maana kabisa.
 
Back
Top Bottom