Wikienda: Penzi ni kama nini?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Nashika tena kalamu
Niseme lilo muhimu
Ya lile lenye utamu

Penzi ni kama ua
likichanua
Nyakua!

Niseme vipi na nene
Kwa dufu tena ninene,
Mwenye macho na aone

Penzi ni kama barua
Huitaji kurarua
Fungua!

Ya nyonda'angu niseme
Nikishindwa niheme
Vinginevyo nihame

Penzi ni kama tunda
Ukilipenda
Panda!

Ya'rabi wangu jalia
Mja wako saidia
Na moyo uje tulia

Penzi ni kama gilasi,
Ukipewa kiasi
Usiasi!

Mtima wangu tetema
Umepewa sasa tama
Kama maji tuwama

Penzi ni kama upepo
Likiwepo
Ni pepo!

Ya konde tena nang'onda
Penzi nimelipenda
Sasa nayeya na nyonda!

Penzi kama maji,
Yupo mpaji,
Usihoji!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 

wonderful
 
Daa,kweli my friday will be murua.Mwanakijiji sikuwezi duu,shairi zuri lakini pia umeniacha hoi jinsi ulivyolipanga,hapo katikati..Aisee uishi mpaka miaka 140....
 
napenzi ya wikiend ni mapenzi ya kudanganyana tuu kwani mapenzi yahajui time or period, ni kitu hakina mwisho na kila siku nimapya .
 
MKJJ

Nimefurahishwa sana na "shape" ya mashairi

Kama hii vile
!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…