Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Nashika tena kalamu
Niseme lilo muhimu
Ya lile lenye utamu
Niseme vipi na nene
Kwa dufu tena ninene,
Mwenye macho na aone
Ya nyonda'angu niseme
Nikishindwa niheme
Vinginevyo nihame
Ya'rabi wangu jalia
Mja wako saidia
Na moyo uje tulia
Mtima wangu tetema
Umepewa sasa tama
Kama maji tuwama
Ya konde tena nang'onda
Penzi nimelipenda
Sasa nayeya na nyonda!
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
Niseme lilo muhimu
Ya lile lenye utamu
Penzi ni kama ua
likichanua
Nyakua!
likichanua
Nyakua!
Niseme vipi na nene
Kwa dufu tena ninene,
Mwenye macho na aone
Penzi ni kama barua
Huitaji kurarua
Fungua!
Huitaji kurarua
Fungua!
Ya nyonda'angu niseme
Nikishindwa niheme
Vinginevyo nihame
Penzi ni kama tunda
Ukilipenda
Panda!
Ukilipenda
Panda!
Ya'rabi wangu jalia
Mja wako saidia
Na moyo uje tulia
Penzi ni kama gilasi,
Ukipewa kiasi
Usiasi!
Ukipewa kiasi
Usiasi!
Mtima wangu tetema
Umepewa sasa tama
Kama maji tuwama
Penzi ni kama upepo
Likiwepo
Ni pepo!
Likiwepo
Ni pepo!
Ya konde tena nang'onda
Penzi nimelipenda
Sasa nayeya na nyonda!
Penzi kama maji,
Yupo mpaji,
Usihoji!
Yupo mpaji,
Usihoji!
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)