Wikiendi Njema: Maombi yangu kwa wanawake wote wa JF wawe wenye kutenda haki na kuwa kwenye unyoofu

Wikiendi Njema: Maombi yangu kwa wanawake wote wa JF wawe wenye kutenda haki na kuwa kwenye unyoofu

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
BINTI YANGU NJOO NIKUAMBIE HAPA.

Mithali 20:7
[7]Mwenye haki aendaye katika unyofu wake, watoto wake wabarikiwa baada yake.

Haki katika ndoa yako ambayo Mungu amekupa hakikisha unaishi katika haki, wamama wengi siku hizi hasa hawa mabinti wanajivunia watoto wao wakiwa wazuri wa sura, wakiwa na akili darasani, na akivaa nguo inamkaa utasikia wanangu wana damu za nguo jamani.

Yaani ndio imekuwa mada yaani umeona watoto wa wengine ni kama vigengedere tu.

Sasa ni hivi mmeacha kuomboleza, mmeacha kumtumikia Mungu, mmeacha kuheshimu ndoa zenu, yaani mmeacha kuwa wenye haki.

Andiko tajwa hapo juu linazungumzia mzazi atakae kwenda ktk unyofu wa haki hakika watoto wake watabarikiwa badala yake, yaani watoto watarithi nini kutoka kwako?

Natamani Ukue uone jinsi gani Dunia imeharibika nje kumeoza ni kwamba Kama jamii haiko salama basi watoto wako hawako salama.

Acha kujipiga msamba tamani kuwa mama muombolezaji na uwafanye watoto wako wana wa Mungu.

Ni maombi yangu watoto wetu wawe wana wa Mungu.
YESU LUGHA YANGU.
 
Mmh Haya sasa mshindwe nyie Pdidy wa bongo ndio kashasema maneno ya busara,
mkimfananisha na yule Mjomba wake Maghayo
P diddy wa kuleee mtajua hamjui huyu kaokaka!
The wise man Did himself ila Mwandiko leo kajitahidi sijui amemwandikia nani ati!
😁😁
Umeamza vizuri unamaliza kama polisi mnataka kunikamata tena ñ yule mdada tushamalizana nae jaman labda waje wengine...
 
FB_IMG_17170934187102315.jpg
 
Pdidy huu mwaka wa matukio athtasahau kamwe wacha Upiteètu
 
Ninakuombea,
Jumamosi yako ikawe ya kujibiwa Sala zako.
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu..
 
Back
Top Bottom