wikiendi ukweni!...

wikiendi ukweni!...

Mi ntaokoa mke kwanza.....mtoto ni majaliwa tu na mungu akipenda tutapata mwingine. Bsbs mkwe na mkewe watabaki wanaokoana wenyewe

ahahaha duh umenifurahisha kweli...kwani mke sio majaliwa wa m.mungu? We naona ungekosa hata huyo mke kama wakwe watabakia wakiokoana.
 
...Interesting! 🙄

...kwahiyo, 'huenda' mwanaume anachokimbilia kuokoa sio mke as mke ila ile 'raha raha' inayotokana na mke! Huyo mke akienda na maji raha yote ya maisha nayo ndio inaishia hapo...!

...or my 'observation' is a bit controversial?

😀

You are very correct Sir, Mbu Sir.
 
kiukweliii, kina mama wengi kwa moyo mweupe tutaenda kwa mtoto sio kwa kuwa tunampenda zaidi ila kwa kuwa ni dhaifu zaidi.
wanawake tunamentality ya kuguswa sana na udhaifu. ndio akili inaenda huko. Ingekuwa baba ni asiyejiweza, mama angapata shida sana kuchagua.

mie ningemuokoa coz nampenda sana sana.....
 
...ndio maana mimi hapo sijaona bado busara ya kumuokoa mke, any way, tuvute subira watu wazidi 'kujikaanga'.
Mbu i like the way ulivyoiweka hii kaka big up

Ila wajameni hamtutendei haki kabisa hapa unaweza kweli kulinganisha mapenzi kwa mtu ambaye umekutana naye ukubwani na yule uliyepata uchungu naye na tabu zote za kumlea? Acheni mchezo najua mtasema mtoto si utampata mwingine bado inauma. Na ni hakika akiulizwa mama yako mzazi kati yangu mie na wewe atasema atakuokoa wewe kwani kama mke utapata mwingine!
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
hii si ni sawa na chicken-egg question kipi kilianza?
 
baba mkwe nae kadata swali gani hilo!!
hajui hata kwake nimeendaa coz ya mtoto wake??
HAPO NAOKOA MKE TUENDELEZE MAISHA
 
...hili swali la wagagagigikoko leo limenikumbusha mbali sana.

img_3526-stilt3.jpg
 
Ningejibu kuepusha ajali kama hii mzee huwa ninahakikisha hatutembei ukoo mzima..., si unajua ajali moja inaweza ikaua kizazi chote.., ? Lakini swali gumu mzee kwani wewe ungenishauri nimuokoe nani.., naomba unifundishe mimi mwanao
 
...lol....VoR nitakunong'oneza usimwambie mtu, sawa? ...jibu utalipata kwa kufikiria upo kwenye stage gani ya mapenzi!
Kama ni mapenzi 'motomoto'...potelea mbali, huoni wala hufikirii mara mbili mbili utalitoa jibu husika...

..Kuna watu kipindi maishani 'waliopendana' hujikuta kwenye hali hii;
hair+dryer.jpg

Hivi baba ku take care ya mtoto kama kumlisha inategemea na heshima anayopata kwa mama??? Nataka ku conclude utafiti wangu kuwa mapenzi ya wababa wengi kwa mtoto ni too conditional, unlike mothers. Sasa mtoto ni wako mimi hata kama ninakufanyia vituko kiasi gani ina husika vipi na wewe kumchukia mwanao??? Yani baba abembelezwe ndio alee mtoto?? Will never beg for that. Ningepata mume wa hivyo wala simshitui ila malipo atayapata mtoto wake akikua kwani ataona kama mtoto atakuwa na mapenzi naye. Yani nikuombe eti baba nanii nisaidie kumpa maziwa mtoto. Nope utajituma mwenyewe; kama unaona hakuna umuhimu I will beter call my housegirl for help not irresponsible father.
 
...lol...Nyumba kubwa swali lako lina ukweli kwa asilimia kubwa sana. Watu watabisha wee, lakini ukweli unarudia pale pale Uchungu wa mwana aujuae mzazi aliyemzaa! ...haya mambo ya unconditional love kwa kiasi fulani yamekaa ki theoretical zaidi.

Uchungu wa kina baba wengi upo kwa watoto wa kike. Ni kama animal instincts hivi...'Competition for survival.'
Wazee wengi linapokuja suala la binti kuolewa, Mzee anakuwa mbogo kwa sababu hata zilizo nje ya msingi.

Halafu kuna ile kumpenda mtoto mmoja zaidi ya mwingine. Kwa wenye watoto zaidi ya mmoja please tusidanganyane hii haijawahi kukutokea,...nazungumzia Kupenda zaidi [sio kutompenda mmoja wapo] kama tutaanza bishana, jichukulie mwenyewe kwenye family yako kama wote mlionyeshwa mapenzi sawa. It's all human nature...
 
...lol....VoR nitakunong'oneza usimwambie mtu, sawa? ...jibu utalipata kwa kufikiria upo kwenye stage gani ya mapenzi!
Kama ni mapenzi 'motomoto'...potelea mbali, huoni wala hufikirii mara mbili mbili utalitoa jibu husika...

..Kuna watu kipindi maishani 'waliopendana' hujikuta kwenye hali hii;
hair+dryer.jpg

Mbu hii ni thread inayojitegemea mydia........stage ya penzi na making choices......lol hapa tutaingia kwenye mengi sana!!
Just out od my curiosity............so kama penzi lime'choka' if I may say so........them possibility ya mke kutoswa ni kubwa eh?? Na je hali ni sawa kwa kina mama?? kuwa kama penzi limechoka ni rahisi kumsacrifice mume eh?
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
Just a quick thought..

kutokana na mapenzi ya ukweli ya mama na mtoto. Automatically Mama ata-influence decision ya baba, yaani Mama/mke hatokubali mtoto afe hata kama baba atakuwa ametaka iwe hivyo. Mama atakuwa radhi kukataa msaada wa baba na kujaribu kuangaika mwenyewe..hatima yake ..Mama na mtoto watakufa. Na kama baba.. utajaribu kumwokoa mtoto..hatapenda kuona mke wake anakufa..Roho itamsuta na ushujaa hata usiowezekana utamwingia..

Scenario yangu ..wote watatu mtakufa..kwani baba atajitahidi kuokoa wote wawili..kitu ambacho hakiwezekani ..lakini kwa wakati huo ..ataona kinawezekana..
 
mmnnnhhh, Mwj1...nimegusia baadhi tu jamani,...
Stages of love zipo, hazikwepeki, ni jukumu la wawili kuhakikisha
mnavuka salama kwenye misukosuko hiyo,...

...Ahhh, acheni mie nijifwaidie na hili penzi la sasa, fainali uzeeni! lol

Just a quick thought..

kutokana na mapenzi ya ukweli ya mama na mtoto. Automatically Mama ata-influence decision ya baba, yaani Mama/mke hatokubali mtoto afe hata kama baba atakuwa ametaka iwe hivyo. Mama atakuwa radhi kukataa msaada wa baba na kujaribu kuangaika mwenyewe..hatima yake ..Mama na mtoto watakufa. Na kama baba.. utajaribu kumwokoa mtoto..hatapenda kuona mke wake anakufa..Roho itamsuta na ushujaa hata usiowezekana utamwingia..

Scenario yangu ..wote watatu mtakufa..kwani baba atajitahidi kuokoa wote wawili..kitu ambacho hakiwezekani ..lakini kwa wakati huo ..ataona kinawezekana..

...Tulizo,..hili swali limelenga zaidi kwenye kutafuta busara ya mhusika, kulikoni kuangalia Consequences za harakati za kuokoa. Ndio maana nikasema swali hili kila mtu anaweza 'kujikaanga kivyake,' lakini madhali upo ukweli huna budi kujibu vile busara na maamuzi yatavyokuruhusu.
 
Back
Top Bottom