Ninafurahi sana ninapoona mtu anayekataa kufuata mkumbo. Ulichoandika ndiyo nimekuwa nafikiria kuhusu hii wikileaks. Marekani inapapatika sasa hivi, haina uhakika adui ni nani na rafiki ni nani, wanajaribu kutingisha kiberiti kuona kitakachotokea. Kwa tunaofuatilia siasa za dunia kwa karibu, tunajua kwa mfano, Ban Ki Moon alipoingia na kumteua Dr. Migiro kuwa msaidizi wake iliraise alarm kwa wakubwa, na mpaka leo naamini wanajiuliza na kuchunguza maana ya uteuzi huo (ikijumuisha uhusiano wa uteuzi huo na connection iliyopo, kama ipo, kati ya S. Korea, N. Korea, Japan na China kwa mfano). Wakati watanzania mnashangilia uteuzi, wengine tulikuwa tunakuna vichwa tukijua kuna wakubwa hawatalala huko).
Hizo habari za kukusanya data za afya za viongozi wa dunia zilisharipotiwa kwenye miaka ya 2002-2003 hivi. Kuhusu S. Arabia na Iran, kama ulivyosema motive inaweza kuwa kuwachonganisha, au kama nilivyosema wanataka kupata undani zaidi wa jinsi hii so-called terrorism inavyoendeshwa, ni tofauti sana na wengi wanavyofikiri, na intelligence ya wamarekani imegundua inaingizwa kwenye mitego.
Binafsi, naamini siasa za ndani za TZ zinachezwa kwa ajili ya watazamaji wa nje ya nchi. Hizo drama za CUF vs CHADEMA vs CCM ni shell game tu. Niliposti hapa wakati wa uchaguzi nikiwaambia watu waache kupoteza muda wao na siasa. Kuna nchi nyingi miaka ya karibuni intelligence community ndiyo zimeingia na zinazoendesha nchi, ikiwemo kuwepo kabisa kwenye vurugu za kisiasa, mfano Pakistani. Kwa mtazamo wangu, TZ ni hivyo hivyo (na hii haimaanishi kila mwanasiasa yupo kwenye intelligence).
Wataongeleaje Zimbabwe na kumuongelea Mbeki kwamba alikuwa bias na kushindwa kumuongelea JK na support aliyoonyesha kwa Mugabe? Wangapi mnakumbuka ule mkutano ambapo baadaye JK alisema 'tutashinda hata kama all odds are against us'? Au ndiyo moja ya mambo walitoblock wikileaks wasi-release? Wangapi walioangalia uchaguzi wa iran na vurugu zilizotokea, katika muelekeo tofauti zaidi tu ya ule wa 'Ahmadinejad na wenzake wameiba kura'?
Wanajaribu kuiintroduce hii Wikileaks kama reliable source of information. Na njia gani nzuri zaidi ya kuonyesha wanaweza kutoa siri za serikali ya marekani? Nia ni siku za mbele kuitumia kuzitikisa na kuzivuruga nchi zingine.
Kuna njia nyingi za kusema uongo na kumanipulate watu, na hawa watu wamefuzu kwenye fani hii.