Wilaya ya Kinondoni, tanuri la kupika viongozi

Wilaya ya Kinondoni, tanuri la kupika viongozi

Ngamanya Kitangalala

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2012
Posts
501
Reaction score
1,214
Wilaya ya Kinondoni kwa miaka ya karibuni imekuwa ni kama tanuri la kupika viongozi kwenye ngazi za juu zaidi

Kumbukumbu zangu za karibuni zinanikumbusha wafuatao

1. Mama Ritta Mlaki, alikuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni na baadaye kuwa mbunge wa Kawe na kuteuliwa na hayati Benjamin Mkapa, kuwa naibu waziri wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi

2. Marehemu Kanali Fabian Massawe, alikuwa mkuu wa wilaya Kinondoni na baadaye Rais Jakaya Kikwete akamteua kuwa mkuu wa mkoa Kagera

3. PauL Makonda, alikuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni, na baadaye hayati Rais Dr John Pombe Magufuli akamteua kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam

4. Ally Hapi, alikuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni, baadaye hayati Rais Dkt. John Pombe Magufuli akamteua kuwa mkuu wa mkoa wa Iringa

5. Comrade Daniel Chongolo , alikuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni, na leo halmashauri kuu ya CCM taifa, imemchagua na kuwa katibu mkuu wa CCM taifa

Wilaya ya Kinondoni imekuwa ni tanuru la kupika viongozi
 
Back
Top Bottom