DOKEZO Wilaya ya Kyela huduma ya Petroli ni changamoto wiki ya tatu sasa, kwani kuna mgomo wa kimyakimya?

DOKEZO Wilaya ya Kyela huduma ya Petroli ni changamoto wiki ya tatu sasa, kwani kuna mgomo wa kimyakimya?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Jamii Forums naomba muwafikishie taarifa kwa Mkurugenzi wa EWURA kuwa wiki ya tatu hatuna mafuta ya Petrol katika Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya.

Nauli zimeanza kupanda, sehemu yakwenda kwa buku sasa hivi ni buku mbili hadi shilingi 2,500.

Kwani kuna nini kinachoendelea wakati kila siku Waziri January Makamba na mamla zinasema hakuna changamoto ya Petrol Nchini?

Ajabu pia wilaya za jirani kama Rungwe huko hakuna changamoto ya Petroli, inadaiwa kuna mgomo wa kimyakimya wakishindika bei ya mafuta ipande.

========================

WAZIRI MAKAMBA ASEMA HAKUNA UHABA WA MAFUTA
Akizungumzia hali hiyo akiwa Mlimani City, Julai 31, 2023, Waziri wa Nishati, Januari Makamba amesema “Hakuna uhaba wa Petroli, tuna mafuta ya siku 15 kama inavyohitajika Kisheria.

"Changamoto za usambazaji zinatokea kutokana na matarajio ya bei, watu wanarudi nyuma kuona kama bei inaweza kupanda, EWURA watafanya doria kuhakikisha mafuta yanafika vituoni na tunatagemea uaminifu wa wafanya biashara katika hilo.

“Kwa wastani kuna Lita Milioni 10 hadi 11 kwa siku zinasafirishwa kutoka Dar kwenda Mikoani, hadi Julai 30 wastani ilikuwa ni Lita Milioni 12 ambayo ni juu zaidi ya ule wastani wa siku zote.”
 
Kama uko Ipinda huko kawaida mafuta yanaisha ndani ya masaa 2

Kingine ni kuwa mafuta yatatolewa Jtano maana bei imepanda kwa zaidi ya 500 hebu pata picha mwenye lita 200 anapiga bei gani hapo

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom