Wilaya ya Rorya imeanzisha program ya kuwafikia Wananchi Vijijini inayoitwa 'POPOTE TUNAKUFIKIA' ambayo imelenga kusogeza huduma karibu na Wananchi ambao hutembea umbali mrefu kufata huduma.
Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka amesisita wataendelea kutekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuendelea kutoa huduma kwa Wananchi, ambapo Wilaya ya Rorya imetenga wiki Moja kila mwezi kushirikiana na Taasisi, Idara na vitengo vyote vitoke kwenda kuhudumia Wananchi.