Tunahitaji watu wenye rekodi nzuri za kiutendaji sio tu kuwa mwanasiasa mzuri tunahitaji watendaji zaidi, nchi yetu imeingia kwenye uchumi wa kati tuache kuishi na kufanya siasa kwa mazoea. Unawezaje kutuletea post ya kumpromote mtu bila kutupa record zake na tabia zake tangu akiwa shuleni mpaka hapo alipo sasa.
Babat mjini na vijijini tumekuwa na wabunge wengi waliopita , lakini wameshindwa kutatua kero za wananchi, mathaliani migogoro ya ardhi kati ya wawekezaji na wanachi. Kuna mashamba yana lease za miaka mingi, na mengine yamekuwa mapori, wananchi wanaongezeka ardhi haiongezeki wananchi hawana ardhi ya kutosha kwa ajili ya kilimo na malisho ya mifugo badala yake wananchi wamegeuzwa kuwa vibarua wa kupalilia miwa na mahindi ya wawekezaji kwa ujira mdogo huku hata wale wanaojitahidi kulima ardhi ndogo iliopo wakikosa maji ya kutosha sababu kiasi kikubwa hutumika kwenye irrigation scheme za wawekezaji.
Ni vyema ungetueleza huyu mgombea amejipangaje kuzitatua kero kama hizi.