Uchaguzi 2020 Wilhelmon Mayo, Mtia nia wa ubunge jimbo la Babati Mjini, Manyara

Uchaguzi 2020 Wilhelmon Mayo, Mtia nia wa ubunge jimbo la Babati Mjini, Manyara

Maendeleo na mabadiliko ya Babati yataletwa na kijana wa Babati ambaye anajua ni nini wanababati wamekosa kwa muda mrefu. Pamoja na kuwa anafanya kazi Babati mjini pia ni kijana mzalendo na anayeshirikiana na wananchi katika maisha ya kila siku. Mtu kama huyo ndio anayehitajika na anayetafutwa na wananchi wa babati mjini.
View attachment 1497699

Tangazo lenyewe tu linamshinda, maandishi kibao kama gazeti la udaku, ubunge hapo itakuwa ngumu
 
Halafu aliyekuandalia hili tangazo bomu kweli. Yaani inabidi kupindisha shingo au kurotate simu ndiyo mtu asome hayo maneno ya mlalo. Rekebisha bana. Andaa bandiko zuri linalosomeka kirahisi
Ndio ujue hata mambo yake ni ya kupindapinda hivyo
 
Maendeleo na mabadiliko ya Babati yataletwa na kijana wa Babati ambaye anajua ni nini wanababati wamekosa kwa muda mrefu. Pamoja na kuwa anafanya kazi Babati mjini pia ni kijana mzalendo na anayeshirikiana na wananchi katika maisha ya kila siku. Mtu kama huyo ndio anayehitajika na anayetafutwa na wananchi wa babati mjini.
View attachment 1497699
Ukiangalia hili tangazo lake utajua ni mzaliwa wa wapi.hata hivyo wewe bado ni mratibu elimu kata,tumikia wananchi kwa nafasi uliyonayo acha tamaaa
 
Maendeleo na mabadiliko ya Babati yataletwa na kijana wa Babati ambaye anajua ni nini wanababati wamekosa kwa muda mrefu. Pamoja na kuwa anafanya kazi Babati mjini pia ni kijana mzalendo na anayeshirikiana na wananchi katika maisha ya kila siku. Mtu kama huyo ndio anayehitajika na anayetafutwa na wananchi wa babati mjini.
View attachment 1497699
babati=Babati
 
Tunahitaji watu wenye rekodi nzuri za kiutendaji sio tu kuwa mwanasiasa mzuri tunahitaji watendaji zaidi, nchi yetu imeingia kwenye uchumi wa kati tuache kuishi na kufanya siasa kwa mazoea. Unawezaje kutuletea post ya kumpromote mtu bila kutupa record zake na tabia zake tangu akiwa shuleni mpaka hapo alipo sasa.

Babat mjini na vijijini tumekuwa na wabunge wengi waliopita , lakini wameshindwa kutatua kero za wananchi, mathaliani migogoro ya ardhi kati ya wawekezaji na wanachi. Kuna mashamba yana lease za miaka mingi, na mengine yamekuwa mapori, wananchi wanaongezeka ardhi haiongezeki wananchi hawana ardhi ya kutosha kwa ajili ya kilimo na malisho ya mifugo badala yake wananchi wamegeuzwa kuwa vibarua wa kupalilia miwa na mahindi ya wawekezaji kwa ujira mdogo huku hata wale wanaojitahidi kulima ardhi ndogo iliopo wakikosa maji ya kutosha sababu kiasi kikubwa hutumika kwenye irrigation scheme za wawekezaji.

Ni vyema ungetueleza huyu mgombea amejipangaje kuzitatua kero kama hizi.

Mbona record yake inajieleza hata kwa kutazama tu picha ni wazi kwamba huyu mkuu alikuwa ni Green guard wa chama, na ametumika kwa muda mrefu katika operesheni mbalimbali za chama kama kusimika bendera za chama mitaani kwa kushirikiana na wafungwa wa magereza.
 
Back
Top Bottom