Freshbrain
Member
- Oct 3, 2011
- 29
- 82
Mr. William Erio ambaye leo ameondolewa katika Cheo cha Mkurugenzi Mkuu NSSF si jina geni. Amekuwa katika cheo kikubwa cha Mkurugenzi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa muda mrefu toka mwaka 2002 alipokuwa Mkurugenzi Mkuu wa PPF hadi mwaka 2018 alipohamishiwa NSSF baada ya kung'olewa Prof. Kahyarara ambaye leo ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Uwekezaji.
Kwa maoni yangu, Erio ni kati ya viongozi walio 'overstay' katika nafasi moja kwa muda mrefu sana, kiasi kwamba inawezekana ubunifu ulikuwa unaelekea au umefika kikomo. Alikaa kama Mkurugenzi Mkuu wa PPF kwa miaka takriban 16 toka enzi za Mkapa hadi enzi za Magufuli. Ukijumlisha na miaka aliyokaa NSSF toka ameteuliwa 2018 inaelekea miaka 20 katika uongozi wa mifuko ya hifadhi ya jamii. Inawezekana aliweza kukaa bila kutikiswa muda mrefu na hata kuendelea kuaminiwa sababu ya mjomba wake Hayati Mkapa (mtakumbuka katika msiba wa ndio alikuwa msemaji wa familia)!.
Pamoja na kwamba kuna wengine mtakuja na hoja kwamba 'experience matters' ila kwa kiongozi wa juu kuoverstay kwa kiasi hicho, kunaleta uwezekano mkubwa wa kutokuwa mbunifu na kuweka 'syndrome' ya kubebana na watu mliokuwa pamoja toka enzi hizo a.k.a ' The Oldboys Club' ili kulinda maslahi yenu yaliyopo kwa muda mrefu.
Hili Erio alilionyesha sana kipindi ameteuliwa kwenda NSSF ambapo licha ya kuhamisha hamisha wafanyakazi lundo waliokuwa wazoefu hapo NSSF na kuwapeleka Serikali Kuu, Halimashauri n.k alihakikisha anabeba viongozi aliokuwa nao PPF na kuhamia nao wote NSSF. Achilia mbali viongozi, ni kama aliihamisha PPF yote kwenda NSSF pamoja na kwamba PPF iliungana na mifuko mingine kuunda PSSSF na hivyo ilibidi asilimia kubwa ya wafanyakazi wake kuwa huko (Ajabu Sana🤔!)
Hii ilipelekea NSSF kutokuwa tena wabunifu na kujikuta inafanya vitu 'kama vilivyokuwa vikifanyika PPF' pamoja na kwamba mazingira ya mifuko hii (operating environment) hayakuwa yanafanana kwa asilimia kubwa kutokana na ukubwa wa mifuko husika na aina ya wateja wake. Hii imeleta usumbufu mkubwa sana kwa wateja katika kipindi cha karibuni na kuchelewesha sana utoaji huduma katika ofisi za mikoa ambapo amepoka mamlaka ya mikoa na maamuzi mengi kufanywa makao makuu. Katika uwekezaji na maeneo mengine nako hali ni hio hio.
Naamini Mr. Masha Mshomba aliyeteuliwa anaenda kurithi hii 'The Oldboys Club' ambapo imeovestay kwa pamoja na Erio, sisemi kwamba awatoe, ila anapaswa kuwa nao makini i.e za kuambiwa changanya na za kwako!.
Namtakia kila lakheri Bw. Mshomba na pia kila la kheri Bw. Erio katika mapumziko yake/kazi mpya na kumpongeza kwa utumishi wa muda mrefu.
Swali kubwa linabaki, je huu ndio mwisho wake? au kuna jema zaidi linakuja?. Wahenga walisema, Muda ni mwalimu mzuri!