July 10, 2017
Wakuu,
Hatua ya Mbunge William M. Ngeleja kuamua kurudisha fedha zenye tuhuma nzito Ths.40,420,000 alizopewa na Ndg. James Rugemalira wa IPTL /ESCROW ni njia mojawapo kujisafisha ili kuweka wazi nafasi ya kuteuliwa tena katika baraza la mawaziri kama Waziri wa Nishati na Madini.
Mheshimiwa Wiliam Ngeleja mbunge wa CCM mwenye taaluma ya sheria na mwakilishi wa jimbo lake la ubunge kwa karibu miaka 12 yaani vipindi vitatu vya kuchaguliwa kama mbunge ana uzoefu wa kibunge, unaibu waziri na waziri kamili katika serikali ya awamu ya nne ya CCM.
Pia katika kupitia hotuba zake na michango Bungeni kwa ''level'' ya CCM kama clip hapa chini anaonesha kuwa na umahiri na unyenyekevu kuliko majigambo ya Prof. Muhongo aliyekuwa Waziri wa Madini na Nishati.
Wizara ya Madini na Nishati ili kuepukana na mikataba mibovu inahitaji waziri mwenye taaluma ya sheria na anayeweza kujenga hoja kwa ''weledi'' mkubwa, kitu ambacho wanasheria wengi huwa ndiyo msingi wa taaluma yao.
Awamu ya tano katika teuzi zake tunaweza kuotea kuwa uteuzi wa waziri wa Madini na Nishati anaweza kutoka CCM bila shaka yoyote na pia katika mikakati ya kuapata kura nyingi zaidi za uchaguzi tunaweza kuotea anaweza kutokea wapi n.k
Tusikilize/ tazame mbunge William Mganga Ngeleja akionesha ''uzoefu'' wake wa sekta ya Madini na Nishati na changamoto za kuweka mabo sawa katika sekata hiyo :
Published on 2 Jun 2017
William Ngeleja Afunguka Issue Ya Mchanga
Source: Global Tv Online

Moderator msaada hamishia jukwaa la siasa