blackstarline
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 3,278
- 7,966
"Kama ilivyo punje moja ya mchanga mbele ya fukwe za bahari kuu za dunia, ndivyo ulivyo ufahamu wetu mbele ya tusiyoyajua duniani na ulimwenguni na mbele ya yale tunayodhani kuwa tunayajua".Huu uwezekano wa Pope kuja siku kulazimisha watu wote waabudu siku moja ya jumapili unautoa wapi?yaani itokee tu siku Papa aamuru kwamba sote Wakristo siku ya kumuabudu Mungu iwe j'pili?
Labda tuseme itabidi iwe vita sasa kwamba anakamatwa msabato kule aliko j'mosi akiabudu kisha analazimishwa kwamba kuabudu ni kesho j'pili utake usitake!hivi kwa akili kidogo tu unadhani dunia hii ya sasa hili litawezekana?au sijaielewa point yako vizuri!
I don't know!
Soma kitabu cha Ufunuo 13...Huu uwezekano wa Pope kuja siku kulazimisha watu wote waabudu siku moja ya jumapili unautoa wapi?yaani itokee tu siku Papa aamuru kwamba sote Wakristo siku ya kumuabudu Mungu iwe j'pili?
Labda tuseme itabidi iwe vita sasa kwamba anakamatwa msabato kule aliko j'mosi akiabudu kisha analazimishwa kwamba kuabudu ni kesho j'pili utake usitake!hivi kwa akili kidogo tu unadhani dunia hii ya sasa hili litawezekana?au sijaielewa point yako vizuri!
I don't know!
TAFASRI YA MNYAMA WA KWANZA WA UFUNUO 13Soma kitabu cha Ufunuo 13...
1 Kisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru.
2 Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.
3 Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.
4 Wakamsujudu yule joka kwa sababu alimpa huyo mnyama uwezo wake; nao wakamsujudu yule mnyama, wakisema, Ni nani afananaye na mnyama huyu? Tena ni nani awezaye kufanya vita naye?
5 Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.
6 Akafunua kinywa chake amtukane Mungu, na kulitukana jina lake, na maskani yake, nao wakaao mbinguni.
7 Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.
8 Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
9 Mtu akiwa na sikio na asikie.
10 Mtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu.
11 Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka.
12 Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.
13 Naye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu.
14 Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi.
15 Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.
16 Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;
17 tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.
18 Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita.
TAFSIRI YA MNYAMA WA PILI WA UFUNUO 13.TAFASRI YA MNYAMA WA KWANZA WA UFUNUO 13
βKisha nikaona mnyama akitoka katika bahari, mwenye pembe kumi, na vichwa saba, na juu ya pembe zake ana vilemba kumi, na juu ya vichwa vyake majina ya makufuru. Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi.β Ufunuo 13:1-2. Mnyama huyu wa ajabu bila shaka anawakilisha utawala wa Rumi. Kumbuka utawala wa Rumi umepitia katika awamu tatu.
Awamu ya kwanza ni Rumi ya kipagani, iliyodumu kuanzia mwaka 168 KK hadi iliposambaratika mwaka 476 BK. Awamu ya pili ni Rumi ya kidini, chini ya papa iliyodumu kuanzia mwaka 538 BK hadi ilipotiwa jeraha la mauti mwaka 1798 BK. Awamu ya tatu na ya mwisho ni Rumi ya kidini ikiambatana na rumi ya kipagani.
Rejea mwanamke aliyekaa juu ya mnyama katika Ufunuo 17. Huo ulikuwa ni utambulisho juu ya huyu mnyama wa ajabu. Katika vichwa vya huyu mnyama kulikuwa na majina ya makufuru.
Tukirudi katika Danieli 7:8 tunaona pembe ndogo iliyochomoza kutoka kwa yule mnyama, yaani upapa, ilinena maneno ya makufuru. Hivyo ni lazima utakuwa ni utawala uleule. Paulo aliligusia hili wakati anazungumzia mtu wa kuasi, βMtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; yule mpingamizi, ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba yeye ndiye Mungu.β 2 Thes 2:3-4.
Uasi ulikuwa umeanza kuingia taratibu katika kanisa hata Paulo akingali hai. Lakini Paulo anasema siku ya Bwana isingaliweza kuja kama hajafunuliwa mtu wa kuasi, ajiinuaye nafsi yake juu ya Mungu. Askofu wa Rumi (papa) anatimiza unabii huu. Makasisi wa kanisa la Rumi wanadai kusamehe dhambi, jambo ambalo ni Mungu pekee anaweza kufanya. Hata Yesu alipofanya hivyo wayahudi walitaka kumpiga mawe kwa madai ya kukufuru, Mathayo 9:3. Mara kadhaa hapo nyuma katika machapisho ya kanisa katoliki, papa anadaiwa kushikilia mahali pa Mungu duniani, kwamba ni mwakilishi wa Mungu. Hivyo kufanya jambo lolote ambalo ni Mungu pekee mwenye uwezo wa kufanya ni kukufuru. Kanisa katoliki linakufuru kwa kudai kuwa na uwezo wa kusamehe dhambi. Linakidhi maneno ya unabii yaliyoandikwa, kwamba kichwani kwa mnyama huyu kulikuwa na majina ya makufuru.
Paulo anaendelea kueleza, βNa sasa lizuialo mwalijua, yule apate kufunuliwa wakati wake. Maana ile siri ya kuasi hivi sasa inatenda kazi; lakini yuko azuiaye sasa, hata atakapoondolewa. Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi,..β 2 Thes 2:6-8. Tumeona kuwa siri ya uasi ilikuwa ikitenda kazi hata wakati wa Paulo lakini kuna mtu alikuwa akizuia uasi huu usifunuliwe kwa mapana yake, ni nani huyu aliyekuwa akizuia? Tumekwisha ona awamu tatu za utawala wa Rumi mwanzoni kabisa mwa hili andiko, na wakati Paulo akiishi ni Rumi ya kipagani ndiyo iliyokuwa na mamlaka chini ya Kaisari. Hivyo ni sahihi kuhitimisha kuwa uwepo wa Rumi ya kipagani katika mamlaka ndiyo nguvu iliyozuia uasi huu usifunuliwe. Historia inaonyesha kuwa mwaka 330 BK Constantine alipohamisha kiti chake cha enzi kutoka mji wa Rome kwenda Constantinople, mji wa Rome ulikabidhiwa kwa askofu wa Rumi (papa). Mwaka 538 BK askofu wa Rumi akawa kiongozi mkuu wa makanisa yote na mrekebishaji wa mafundisho ya uongo. Hivyo kiti cha Rumi kilikaliwa na papa; na mamlaka ya papa yalitoka kwa yule joka.
Tukidumu katika fungu la pili, tunaona mnyama huyu alikuwa kama chui, alikuwa na miguu kama ya dubu na mdomo kama wa simba. Mnyama huyu alikuwa na tabia zote za wanyama wale wa Danieli 7. Kwa maneno mengine ni kwamba utawala huu ulikuwa na tabia za tawala za nyuma zilizopita. Chui aliwakilisha utawala wa uyunani (ugiriki). Tunaona miungu mingi ya kigiriki iliendelea kuabudiwa na rumi, majina tu ndiyo yaliyobadilika. Mfano mungu wa miungu yote ya kigiriki aliitwa Zeus. Ni huyu ambaye kwa warumi aliitwa Jupiter, jina ambalo ilipewa sayari kubwa kupita zote. Huo ni mfano mmoja tu, lakini kuna miungu mingi na taratibu nyingi za ibada zilizoazimwa kutoka ugiriki. Dubu aliwakilisha umedi na uajemi. Sifa kuu ya utawala wa umedi na uajemi ilikuwa kwamba sharia iliyopitishwa haiwezi kubadilika kwa namna yoyote ile. Rumi pia inayo hiyo sifa. Hata ile pembe ndogo (upapa) katika Danieli 7:8 tunaona ilikuwa na macho na mdomo lakini haikuwa na masikio. Hii ni kielezo kuwa Rumi ni ile ile leo na hata kesho. Simba aliwakilisha utawala wa Babeli. Ibada ya jua iliyofanyika katika Babeli yaa zamani iliendelea hata katika Rumi japo kwa namna na majina mengine.
βNikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia mnyama yule.β Ufunuo 13:3. Pigo la mauti hapa linawakilisha ukomo wa utawala wa papa mwaka 1798 BK ambapo jenerali Berthier, kwa amri ya Napoleon, aliingia Vatican na kumteka papa Pius VI na kumpeleka uhamishoni ambapo alifia huko mnamo mwaka 1799 BK. Likatimia neno la Ufunuo 13:10 βMtu akichukua mateka, atachukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga.β βNaye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uwezo wa kufanya kazi yake miezi arobaini na miwili.β Fungu la 5. Miezi arobaini na miwili inayotajwa hapa ndiyo miaka mitatu na nusu kwenye ufunuo 12 na ndiyo siku 1260 ambazo utawala wa papa ulipewa upate kufanya kazi yake na kuwatesa watu wa Mungu. Tukitumia kanuni ya siku sawa na mwaka (Ezekieli 4:6) tunapata miaka 1260. Hii ilianza mwaka 538 BK hadi mwaka 1798 BK upapa ulipopata pigo la mauti. Katika kipindi hiki mamilioni ya wakristo walipoteza uhai wao kwa amri ya askofu wa Rumi.
Pigo la mauti lilipona! Papa Pius VI alipofia uhamishoni huko ufaransa watu wakadhani kuwa mwisho wa upapa umefika, lakini kama andiko lilivyosema, mwaka 1929 BK Benito Mussolini aliingia makubaliano na upapa na kuitambua Vatican kama nchi huru, hivyo mamlaka aliyokuwa nayo papa kama kiongozi wa nchi na dini yakarudi, na kwa kufanya hivyo jeraha lake la mauti likawa limepona. Na hadi leo Papa ndiye kiongozi wa dini zote duniani na pia ni kiongozi wa Vatican kama nchi.
TAFSIRI YA MNYAMA WA PILI WA UFUNUO 13.
βKisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka.β Ufunuo 13:11. Bwana Wesley, katika maelezo juu ya Ufunuo 13 aliyoandika mwaka 1754, akizungumzia mnyama mwenye pembe mbili; βHajaja bado, japo hawezi kuwa mbali sana: kwa maana amekusudiwa kuonekana mwishoni mwa miezi arobaini na miwili ya yule mnyama wa kwanza.β
Mnyama wa kwanza alipanda kutoka kwenye bahari, ambayo inaonyesha kuinuka kwake kutoka katika watu wengi na mataifa mengi ya wakati huo (Ufunuo 17:5), wakati huyu wa pili anainuka kutoka katika nchi. Hii inaonyesha kuwa mnyama wa pili angetokea mahali ambapo hapakuwa na watu wengi, wala mataifa, lugha na jamaa. Mwaka 1798, wakati mamlaka ya kipapa yalipotiwa jeraha la mauti, utawala wake ulienea maeneo yote muhimu ya Ulaya, Asia na Afrika; na mahali pekee kwa ajili ya mnyama wa pembe mbili kuendelea palikuwa ni bara la magharibi. Tukilitazama hili bara tunaona marekani ndilo taifa huru lililokuwa na idadi ndogo ya watu kwa wakati huo. Taifa la Marekani lilijitangazia uhuru wake kutoka kwa mkoloni mwingerza tarehe 4 Julai 1776. Hivyo wakati papa Pius VI akichukuliwa kwenda uhamishoni, taifa la Marekani lilikuwa likikua na kujiimarisha.
Pembe huwakilisha utawala au sehemu ya utawala, kama ilivyoainishwa katika Danieli 7:7, 8, 24, 25. Pembe kama za mwana-kondoo zinaonyesha uchanga, kutokuwa na hatia na upole. Soma Great controversy, 442. Pembe mbili zaweza kuwakilisha kanuni zilizoongoza serikali, uhuru wa kisiasa na kidini.
Mbali na kuwa na pembe mbili kwa maana kwamba dini na serikali ni vitu viwili tofauti, mnyama huyu baadae alikuja kunena kama joka! βNaye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.β Ufunuo 13:12. Sifa kuu ya upapa ilikuwa ni kuunganisha dini na serikali. Kanisa lilipoasi huko zamani likatafuta msaada kwa serikali na hivyo kutumia serikali kuwaadhibu wale ambao walijaribu kwenda kinyume na mafundisho ya kanisa. Ndipo tunasema upapa ulipata nguvu na mamlaka kutoka kwa yule joka. Joka aliwakilisha Shetani lakini kupitia serikali ya Rumi.
Taifa la marekani lilikuwa taifa la kiprotestanti tangu kuanzishwa kwake, na lilikuwa kimbilio kwa wakristo ambao walikimbia mateso kule Ulaya. Ni taifa ambalo lilikuwa na uhuru wa kidini, uhuru wa dhamiri, serikali haikuingilia mambo ya dini. Tarehe 7 Januari 1984, Raisi wa Marekani aliyekuwa madarakani, Ronald Reagan, alimteua balozi kuiwakilisha Marekani huko Vatican; huo ukawa mwanzo wa kujenga mahusiano baina ya Marekani ya kiprotestanti na upapa. Tangu hapo mahusiano baina ya pande hizi mbili yamekuwa yakiimarika siku baada ya siku ikiwemo viongozi kutembeleana. Na kama ilivyotabiriwa; katiba ya marekani imekuwa ikifanyiwa marekebisho kwa zaidi ya mara kumi na nne, lengo na kusudi ni kuondoa uhuru wa dhamiri, uhuru wa kidini, kuunganisha dini na serikali na hivyo taifa la Marekani lililokuwa la kiprotestanti litakuwa limefuata nyayo za Rumi na litakuwa limenena kama joka.
βNaye afanya ishara kubwa, hata kufanya moto kushuka kutoka mbinguni uje juu ya nchi mbele ya wanadamu.β Ufunuo 13:13. Taifa la Marekani limekuwa kituo cha ishara na miujiza. Wahubiri wengi wenye kufanya miujiza wametokea katika taifa hili. Kunena kwa lugha kunakofanywa leo miongoni mwa wakristo kulianzia Marekani mwanzoni mwa miaka ya 1900. Watu wanadai kushukiwa na Roho mtakatifu lakini ukweli ni kwamba moto unaowaka ndani ya hawa watu siyo moto wa mbinguni bali ni moto wa kigeni! Vuguvugu la karismatiki ambalo linaenea kwa kasi miongoni mwa wakatoliki pia limeanzia katika taifa hili. Vuguvugu la kizazi kipya na wahubiri wakubwa wa mambo hayo chanzo chao ni Marekani. Dini nyingi za siri zinazomwabudu Lusifa zimeanzishwa katika taifa hili.
βNaye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi. Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe.β Ufunuo 13:14-15. Juu ya sanamu ya mnyama, Ellen G White anaandika, βsanamu ya mnyama inawakilisha namna ya uprotestanti ulioasi ambao utaundwa wakati makanisa ya kiprotestanti yatakapotafuta nguvu ya serikali kwa ajili ya kushurutisha watu wafuate mafundisho yao ya diniβ The great controversy ukurasa wa 445.
βNaye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao; tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.β Ufunuo 13:16-17. Baada ya makanisa ya kiprotestanti kuungana katika baadhi ya vipengele vya mafundisho ambavyo wanafanana hasa hasa ibada ya jumapili, yatashinikiza serikali kuweka sheria kwa kuifanya jumapili kuwa siku ya mapumziko na adhabu kutolewa kwa wale ambao watakiuka agizo hilo.
Kutiwa chapa katika mkono wa kuume ni kukubali kutii agizo kwa kutofanya kazi. Katika vipaji vya uso ni kusadiki au kuamini ya kwamba agizo hilo ni halali. Funuo 13:18, hesabu ya mnyama ni namba 666. Kofia ya papa imeendikwa kilatini "VICARIUS FILII DEI" ambayo tafasiri yake ni Vicar of the Son of God. Maana yake ni aliye badala ya Mwana wa Mungu. Ukilinyambulisha hilo neno VICARIUS FILII DEI kwa kutumia herufi za kirumi unapata jumla ya namba 666.
hivi huyo mwanazuoni na Yesu nani yuko karibu na Mungu? Tuanze kujadili kutokea hapo
Nyie Wasabato mpoje? Huo ndio UPINGA KRISTO ,Yesu alisema jihadharini na manabii wa Uongo Sasa wewe unaona hakuna shida kutafsiri au kutabiri uongoKukosea kutafsiri unabii siyo dhambi...hata wayahudi hawakuulewa unabii wa ujio wa Yesu, walikuwa wanamsubiri masihi mwingine. Hata wanafunzi wa Yesu walikuwa wanajua kuwa Yesu anakuja kusimika ufalme wake duniani, na ndiyo maana alivyowaambia anaenda zake mbinguni hawakumuelewa.
Pointi ni kwamba, huo unabii ulikuwa unalenga tukio fulani, lakini si kama yeye alivyoelewa, swali ni kwamba nyie mnaombeza Miller mnatoa tafasri gani ya huo unabii?
Umeandika kiushabiki sana. Lengo lako ni kuwaattack wasabato na wala si vinginevyo.
Mambo mengi uliyoeleza hapa si ya kweli, kama ifuatavyo.
1. Miller haukuwa msabato na hata kipindi akiwa anahubiri kurudi kwa Yesu, hapakuwa na dhehebu la kisabato.
2. Mama White pia hakuwa msabato kipindi hicho maana hapakuwa na hilo dhehebu, na wala hakuwa mwanzilishi wa hiyo kanuni ya kurudi Yesu unayoisema, isipokuwa alikuwa mfuasi wa Miller.
3. Papa hatawafumusha wasabato kusali jumamosi kama ulivyodai, badala yake atawalazimisha watu wote kusali siku ya kwanza ya juma (yaani Jumapili) badala ya siku ya saba ya juma (yaani Jumamosi).
4. Yesu yuko katika chumba cha patakatifu pa patakatifu mbinguni akifanya huduma ya uombezi, na si kwamba ameshaanza kushuka kuja duniani kama unavyodai. Maana patakatifu pa patakatifu ni mbinguni.
5. Wasabato hawaja set siku yoyote ya kuja kwa Yesu kama unavyotaka kuwaaminisha watu, badala yake wamaamini kwamba Yesu amekaribia sana maana dalili karibia zote zimeshatimia.
6. Pamoja na kukosoa mahesabu ya Miller kuhusiana na unabii wa Daniel wa siku 2,300, hujatoa tafsiri mbadala wa unabii huo kana k
kwamba unabii huo hauna maana yoyote kwa wanadamu wa leo.
7. Ukweli ni kwamba, mahesabu ya Miller yalikuwa sahihi, kwamba mwaka 1844 kulikuwa na tukio kubwa lilikuwa linaenda kutokea. Kosa la Miller ni kwamba, alitafasri vibaya kuwa hekalu ni dunia na kutakaswa kwa Hekalu ni dunia kusafishwa kwa moto (kama ulivyoelezea vizuri kabisa).
Ukitaka kujua tafasri ya huo unabii wa siku 2,300 unakaribishwa kuuliza.
Aisee...atatoka lini humo chumbani? Yaani ni ngumu sana kufuta spiritual mistakes za mtu bila kumkana. Kwanini msiseme miller na Helen walikosea...halafu nyinyi mkafata njia sahihi hii cover ups haiwajengi inazidi kuwaboboa. Miller na hellen bi simba destroyed you big time...mtupeni pembeni muendelee na imani sahihiFundisho Kuhusu Patakatifu pa Duniani ,Na Jinsi linavyoakisi Huduma ya Yesu Katika Patakatifu pa Mbinguni
Katika Biblia patakatifu pa duniani ni mfano wa patakatifu pa mbinguni. Paulo anapaita patakatifu pa duniani kuwa ni kivuli cha Mambo ya Mbinguni. Biblia yasema hivi;β-watumikiao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa mfano ule ulioonyeshwa katika mlima. [Waebr8:5]. Hivyo Basi tunaona Ukweli Ufuatao
1. Patakatifu pa duniani ni mfano wa patakatifu pa mbinguni. Patakatifu pa mbinguni ni kitu halisi ambapo patakatifu pa duniani ni kivuli chake, ama mfano wake.
2. Patakatifu pa duniani palikuwa na Hema mbili zilizotenganishwa kwa pazia katikati, Hema ya kwanza iliitwa patakatifu, na Hema ya pili iliitwa Patakatifu Mno. [Tazama Ebr9:2-3].
3. Hema ile ya Kwanza iitwayo Patakatifu palikuwa na vitu vifuatavyo. Palikuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate ya Wonyesho, na madhabahu ya dhahabu ya kufukizia uvumba;Tazama Kut40:22-27,Tazama pia Waebr9:2]
4. Hema ile ya Pili iliyiitwa Patakatifu mno ilikuwa na vifuatavyo;β-Chetezo cha dhahabu,Sanduku la Agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote,Kopo la Dhahabu lenye Mana, Fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao viwili vya Agano,[Taz Ebr9:3-5].
5. Katika ile Hema ya kwanza iitwayo Patakatifu, Makuhani waliingia kila siku, Lakini katika Ile Hema ya Pili iitwayo patakatifu Mno Kuhani Mkuu aliingia mara moja kwa Mwaka.[TazamaEbr9:6-7].
6. Huduma za kutoa kafara zilizokuwa zinafanyika kila siku Asubuhi na Jioni daima katika Ile hema ya kwanza iitwayo patakatifu zilikuwa zinafanyika ifuatavyo. Mdhambi alikuwa anakuja na mnyama wake awe kondoo ama ngβombe mkamilifu, anamleta mbele ya kuhani katika ile Hema ya kukutania. Na kisha anaweka mkono wake juu ya mnyama na kuziungama dhambi zake zote juu ya mnyama yule. Mnyama yule anafungwa na kuwekwa juu ya madhabahu na kisha mdhambi anaagizwa amchinje. Kisha Kuhani aliyetiwa mafuta anaitwaa baadhi ya damu ya yule mnyama na kuingia nayo hadi patakatifu na kisha anainyunyiza juu ya mapazia ya hekalu na juu ya madhabahu ya kufukiza uvumba. Hivyo kwa njia ya damu dhambi zilizotubiwa za mdhambi zinaamishwa hadi patakatifu kwenye mapazia ya hekalu. Na Baada ya hapo yule mnyama alikuwa anateketezwa kwa moto. Tazama[Wal4:1-11].
7. Huduma za kutoa makafara zilizokuwa zikifanyika mara moja kwa mwaka katika ile Hema ya pili iitwayo Patakatifu Mno ilikuwa kama ifuatavyo. Mara moja kwa Mwaka ilikuwa inaitwa Siku kuu ya upatanisho. Wana wa Israeli wote walikusanyika mbele ya Hema ya kukutania, wakijichunguza nafsi zao na kuziungama dhambi zao mbele za Mungu. Kuhani Mkuu akiisha kufanya Upatanisho wa nafsi yake Mwenyewe, Walichaguliwa Mbuzi wawili wakamilifu na kupigiwa kura ili apatikane Mbuzi wa Bwana na Mbuzi wa Azazeli. Yule aliyeangukiwa kuwa Mbuzi wa Bwana, anachukuliwa na kufanywa sadaka ya dhambi.Mnyama yule anachinjwa na Kuhani anaichukua Damu ya yule mnyama na kuingia nayo patakatifu mno, na kuinyunyiza juu ya kiti cha Rehema, na mbele ya kiti cha rehema, na kisha atatoka nje na ile damu na kuinyunyiza juu ya madhabahu iliyo mbele za Bwana. Hivyo kwa njia hiyo machafu yote ambayo yalikuwa yakihamishwa kwa njia ya damu hadi mle kwenye Hema ya kwanza iitwayo patakatifu yalitoka yote na kuwa juu ya mikono ya kuhani. Na kisha kuhani alimchukua yule mbuzi wa Azazeli na kisha kuziungama dhambi zile zote za Mkutano wa wana wa Israeli juu ya mbuzi wa Azazeli. Na kisha anachaguliwa Mtu ambaye atamchukua Mbuzi wa Azazeli na kwenda naye mpaka jangwani na kumwacha huko. Hivyo ndivyo Patakatifu palivyotakaswa katika Hekalu la zamani. [Tazama Wal16:1-34]
8. Kama tulivyoona Mwanzoni kuwa patakatifu pa kale pa kidunia palikuwa ni mfano ama kivuli cha patakatifu pa mbinguni, na Musa aliagizwa kutengeneza patakatifu pa kidunia kwa mfano wa patakatifu pa mbinguni kama alivyoonyeshwa. Hivyo kwa maana nyingine ni kwamba patakatifu pa mbinguni ndipo patakatifu halisi, na ambapo pa dunia ni mfano wake. Hivyo mfumo wa patakatifu pa duniani ni taswira na mfanano wa patakatifu pa mbinguni.
9. Swali ka Kujiuliza ni kwamba Je Mbinguni kuna patakatifu[ Santuary]? Na kama lipo linafananaje?
10. Biblia iko wazi kuwa Mbinguni kuna patakatifu, ile hema ya kweli ambayo imefanyika pasipo mikono ya Mwanadamu ambamo Yesu amekwenda kuhudumu kwa ajili yetu. Biblia yasema hivi;β-Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni, mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu. [Ebr8:1-2].
11. Nabii Yohana alionyeshwa Mlango wa Hekalu la Mbinguni ukifunguliwa, Akaonyeshwa ile Hema ya Kwanza iitwayo patakatifu na akamwona Mungu akiwa ameketi kitini pa enzi akizungukwa na Wazee ishirini nan ne, na wale wenye Uhai wanne. Mbele zake zinawaka taa saba za Moto na ndizo Roho saba za Mungu. Taz Ufu4:5]. Tunatambua kuwa hapa ni ile hema ya kwanza iitwayo patakatifu sababu zle taa saba za Moto katika patakatifu pa duniani ziliwakilishwa na kile kinara cha taa chenye taa saba. Katika Kitabu cha Ufunuo 8;3-5, tunaona madhabahu ya dhahabu ya kufukiza Uvumba iliyo mbele za Bwana, chetezo cha kufukiza uvumba, Madhabahu ya dhahabu ya kufukizia Uvumba ilikuwepo katika ile Hema ya kwanza iitwayo Patakatifu.
12. Nabii Yohana alionyeshwa pia Hekalu lililoko mbinguni likifunguliwa tena na kisha akaona Sanduku lile la Agano lenye kubeba Amri kumi. Hapa Nabii alionyeshwa ile Hema ya pili iitwayo Patakatifu mno. Sanduku la Agano katika Hekalu la Kidunia lilikaa patakatifu Mno.Biblia yasema hivi;β-Kisha Hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua ya mawe nyingi sana. [Ufu11:19]
13. Hivyo basi tunaona kuwa kama patakatifu pa kidunia palivyo na sehemu mbili ambazo zinatanganishwa na pazia yaani patakatifu na patakatifu Mno, hali kadhalika na patakatifu pa mbinguni pana sehemu mbili ambazo ni Patakatifu na Patakatifu mno.
14. Hebu sasa tuangalie Mfanano wa huduma kama zilivyokuwa zikifanyika katika patakatifu pa duniani na patakatifu pa mbinguni.
15. Katika patakatifu pa kidunia makuhani ama kuhani Mkuu aliingia patakatifu kwa damu ya wanyama ili kuwafanyia wana wa Israeli upatanisho. Katika patakatifu pa mbinguni Yesu anaingia kwa damu yake mwenyewe ili kuwafanya watu wake upatanisho. Biblia yasema hivi;β- wala si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika Patakatifu, akiisha kupata ukombozi wa milele. [Ebr9:12]
16. Katika Patakatifu pa duniani, Kiti cha rehema na Sanduku la Agano lilikaa katika Ile hema ya pili iitwayo Patakatifu mno, Lakini Utukufu wa Mungu ulipopashukia Patakatifu mno na kukaa juu ya kiti cha rehema, Utukufu wa Mungu ulipajaza mahala pote patakatifu na patakatifu mno, kama ishara kuwa Uwepo wa Mungu unapatikana kote kote iwe ni Patakatifu ama iwe ni patakatifu mno. Hali kadhalika na katika patakatifu pa mbinguni Mungu anaonekana katika Hema zote mbili iwe ni patakatifu ama patakatifu mno.[Tazama Kut40:34]
17. Kila Siku daima, Makuhani waliingia Patakatifu wakiwa na damu ya mnyama ili kufanya upatanisho, Hali kadhalika na Kristo baada ya kupaa na kwenda mbinguni, alikwenda kukaa mkono wa kuume wa Mungu na kuanza kazi yake ya kuwafanyia watu wake upatanisho na kuwaombea. Biblia yasema hivi;β-Basi, katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye kuhani mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Ukuu mbinguni, mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu. [Ebr8:1-2].
18. Mara moja kwa Mwaka Kuhani Mkuu aliingia patakatifu mno ili kupatakasa patakatifu. Hali kadhalika na Kristo Aliingia patakatifu mno Mwaka 1844 AD, ili kupatakasa Patakatifu kulingana na unabii wa Daniel wa siku 2300 ambao ni sawa na Miaka 2300.Unabii unasema kuwa Mwishoni mwa siku 2300 ndipo patakatifu pataakaswa. [Tazama Dan8:14.]
19. Katika Patakatufu pa kidunia, Baada ya Mdhambi kumchinja mnyama, Kuhani aliichukua ile damu na kisha kuinyunyiza katika mapazia ya Hekalu, na hivyo kwa njia ya damu Dhambi za mdhambi aliyetubu kuhamishwa katika mapazia ya hekalu kama kumbukumbu ya dhambi zake, zikisubiri kusafishwa mara moja kila Mwaka. Katika patakatifu pa mbinguni, dhambi zote za watakatifu zilizosamehewa na kutubiwa, zinarekodiwa katika vitabu vya mbinguni, pamoja na ushahidi wa toba yake ya dhati, vikisubiri kuja kuondolewa kwa umilele wakati wa kazi ya Yesu katika ile hema ya pili iitwayo patakatifu mno. Musa alipowaombea wana wa Israel aliomba hivi;β- ;β-Walakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao - na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichoandika.[Kut32:32]. Lakini Jibu la Mungu likawa hivi;β-Bwana akamwambia Musa, Mtu ye yote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu. [Kut32:33].Pia soma Ufu20:12.
20. Mara moja kwa Mwaka katika patakatifu pa kidunia Kuhani mkuu aliingia Patakatifu Mno na damu ya Mbuzi ili kupatakasa patakatifu. Mbuzi wawili walipigiwa Kura mmoja awe wa Bwana na Mwingine awe wa Azazeli. Mbuzi wa Bwana alichinjwa na kuhani aliichukua damu ya mnyama na kuinyunyiza juu ya kiti cha Rehema, na mbele ya kiti cha rehema, na hivyo dhambi zote zilizokuwa zikihamishwa ndani ya ile hema ya patakatifu kwenye mapazia ya Hekalu zilikuwa zinaondolewa zote na patakatifu panatakaswa na dhambi zote zinakuwa juu ya mikono ya kuhani. Na kisha anachukuliwa yume Mbuzi wa Azazeli na Kisha kuhani anaweka Mikono yake juu ya Mbuzi wa Azazeli. Hivyo machafu yote ya wana wa Izraeli yalitoka kwenye Mikono ya kuhani hadi kwa Mbuzi wa Azazeli, na kisha Mtu aliyewekwa tayari aliagizwa amchukue Mbuzi huyo na kwenda naye jangwani na kumuacha huko. Hali kadhalika na Patakatifu pa mbinguni, Nabii Danieli alionyeshwa kuwa Mwishoni mwa siku 2300 ambayo ni sawasawa na Miaka 2300, ambazo kulingana na Unabii ziliishia mwaka 1844 AD, Yesu aliingia Patakatifu Mno pa Mbinguni ili kupatakasa patakatifu. Tokea Mwaka huo vitabu vya mbinguni vimekuwa vikikaguliwa na kuchunguzwa, na wale watakatifu waliotubu katika Damu ya Yesu dhambi zao zinafutwa milele, na majina yao yanadumishwa katika kitabu cha Uzima. Lakini wale watakatifu ambao wataonekana kuwa kuna dhambi ambayo haikutubiwa, basi dhambi zao hazitafutwa hata milele na majina yao yatafutwa yatoke katika kitabu cha Uzima. Dhambi ambazo watakatifu walizitenda zitafutwa na zitawekwa mikononi mwa Yesu, na kazi yake katika patakatifu pa mbinguni ikiisha, ndipo ataziweka dhambi zote ambazo watakatifu walisababishiwa kuzitenda juu ya Shetani, na Shetani atafungwa hapa duniani na malaika zake mda wa Miaka Elfu, akisubiri Uangamivu wake wa Mwisho. Kazi ya Yesu katika patakatifu mno mbinguni ikiisha, Anapewa Ufalme, na idadi ya waliokombolewa inakamilika. Yesu atarudi kuwachukua watakatifu.
21. Nabii Danieli alionyeshwa Baba akihama toka patakatifu na kwenda patakatifu mno kwa kiti chake cha Enzi cha Moto na chenye Magurudumu ya moto. Alionyeshwa malaika Maelfuelfu wakisimama mbele zake na kumtumikia. Alionyeshwa vitabu vya mbinguni vikifunguliwa na kuchunguzwa, na Upinga Kristo uliovaa vazi la Udini ukihukumiwa. Biblia yasema hivi;β- Nikatazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa. [Dan7:9-10].
22. Nabii Daniel alionyeshwa Yesu akija na Mawingu ya Mbinguni, sii kuja hapa duniani, bali akimkaribia mzee wa siku huko Patakatifu mno mbinguni, ili kumalizia kazi yake ya Mwisho ya Upatanisho katika patakatifu pa mbinguni, na kusimama kama mtetezi wa watakatifu wakati rekodi zao zinapokaguliwa mbele za Baba. Kazi yake ikiisha anapewa ufalme, na kisha anakuja kuwachukua watakatifu. Biblia yasema hivi;β- Nikaona katika njozi za usiku, na tazama, mmoja aliye mfano wa mwanadamu akaja pamoja na mawingu ya mbingu akamkaribia huyo mzee wa siku, wakamleta karibu naye. Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa. [Dan7:13-14]
Hii ni mpya...yesu anaomba sisi tusamehewe au yeye ndo anatusamehe dhambi. Mkuu unaenda OP sana. Ndiyo maana watu huwema wasabato si wakristo..naona mnaspiritual flaws nyingi kuliko nilivyodhani mwanzoni. Kosa kubwa ni kuchukua mawazo ya mtu na kuyafanya ndiyo msimamo wa imani. Hellen amwkuwa kama Mao na red bookAnawaombea watenda dhambi kwa Baba yake. Mtu anapoomba msamaha wa dhambi, Yesu anayapeleka maombi hayo kwa Baba yake kwa ajili ya msamaha.
Kuhusu kusali jumapili zitto junior alifafanua vizuri sana ktk ile mada ya mitale na midimu ya kuumbwa kwa siku ya saba hapa huna jipya.Unashadadia sana ukatoliki bila kujua unaabudu nini? Kwa taarifa yako Mungu hakuanzisha ukatolik, ni mfalme mpagani constantine ndiye aliyeleta ibada ya Jumapili na mafundisho mengine ya kipagani. Na wewe eti unajisifu kwa kuwa mkatoliki, hujui unachokiamini. Nina mambo mengi ya kusema lakini sitaki kuwakwaza watu hapa na imani zao, ila unataka kuniprovoke!
Msubiri tuwaoneshe jinsi Ellen G White alivyopinga Utatu Mtakatifu mpaka GC kuficha nyaraka zakeπππ perfect umeeleza vzr sana lengo kuu ni kuwaattack wasabato akidhani hawana ushahidi na uelewa wa kupinga hayo maneno yake
Wanafanya hivyo kwa kuwa Ellen G White alimfananisha Yesu na Malaika Mikaeli..Hii ni mpya...yesu anaomba sisi tusamehewe au yeye ndo anatusamehe dhambi. Mkuu unaenda OP sana. Ndiyo maana watu huwema wasabato si wakristo..naona mnaspiritual flaws nyingi kuliko nilivyodhani mwanzoni. Kosa kubwa ni kuchukua mawazo ya mtu na kuyafanya ndiyo msimamo wa imani. Hellen amwkuwa kama Mao na red book
Hivi hujui Ellen G White alisema Yesu sio Mungu ila Malaika Gabrieli...πππ perfect umeeleza vzr sana lengo kuu ni kuwaattack wasabato akidhani hawana ushahidi na uelewa wa kupinga hayo maneno yake
Mimi sikuona huo ufafanuzi...labda kama unayo niletee hapa nitakujibu...hakuna justification ya kibiblia ya kusali JumapiliKuhusu kusali jumapili zitto junior alifafanua vizuri sana ktk ile mada ya mitale na midimu ya kuumbwa kwa siku ya saba hapa huna jipya.
Una ushahidi wa kile ulichokisema? Kama unao tupia hapa.Hivi hujui Ellen G White alisema Yesu sio Mungu ila Malaika Gabrieli...
Tembelea JF tutakujuza
Ndio ukae mkao wa kula....Una ushahidi wa kile ulichokisema? Kama unao tupia hapa.
Huo ni uongo...hakuna sehemu EGW alipinga kuwa Yesu si Mungu. UONGO. Biblia inamtaja Yesu kuwa Mikaeli, malaika mkuu, lakini haimanishi kuwa Yesu si Mungu. Hilo ni jina lake jingine kama alivyoitwa mwana kondoo wa Mungu, au simba wa Yuda. Usipotoshe watu.Hivi hujui Ellen G White alisema Yesu sio Mungu ila Malaika Gabrieli...
Tembelea JF tutakujuza