William Oduol, mgombeaji wa Ugavana Siaya, ampa mkewe kibano cha kutisha...picha zinasikitisha!

William Oduol, mgombeaji wa Ugavana Siaya, ampa mkewe kibano cha kutisha...picha zinasikitisha!

pics-1-001.jpg



Mkuu kiongozi wangu Mchina,

Ingawaje natambua wajibu wangu wa kuheshimu mawazo yako hata kama siyapendi lakini katika sura nilioiona hapo pichani juu, kamwe siungi mkono hata kidogo wazo lako la eti KUTAZAMA NA UPANDE WA PILI hapa.

Huyu jamaa ni mtu mkatili, mshamba na mchafu wa tabia asiyestahili hata kidogo kugombea hata nafasi ya ubalozi wa nyumba kumi.

Japo tukio limetokea nchini Kenya, lakini nichukue fursa ya kuviomba vyamba vyetu vyote vikiwemo CUF, CHADEMA, CCM, TLP, NCCR-Mageuzi na vyama vinginevyo kwamba ni waakati mwafaka kuchagua KULINDA HESHIMA NA HADHI YA MWANAMKE NA MTOTO katika jamii yetu kwa kuingiza kigezo rasmi mojawapo kwenye katiba mpya ijayo kwamba yeyote mwenye kosa, hulka na tabia ya kusababishia madhara ama ya kimwili, kifedha au kisaikolojia asiweze kushika nafasi yoyote katika ofisi za umma endapo mtu yeyote anaweza kweli akajitokeza na uthibitisho wa kuaminika dhidi yake.

Hakika nimesikitishwa sana moyoni juu ya (1) madhara ya kimwili aliyosababishiwa mama huyu, (2) kuonekana kuzulumika kwa kutumika kimwili na kutupwa pembeni kama dodoki na mwaname mchafu huyu kabla ya kumdandia mdhaifu wake mwingine ambaye naye huenda akatendwa vivi hivi tu hapo mbeleni, na mbaya zaidi (3) ni kule kumfanya mama huyu akose ajira yake kwa kushindwa kufika kazini kutokana na maumivu makali mno mwili.

Laiti ingalikua ni kwamba jambo hili lilitokea hapa kwetu huyu mwanamme angejuta kuzaliwa pindi angekutana na akina mama zetu 'Simba Jike lenye watoto wachanga' kama vile Mama Ananilea Nkya na mama Kijo Bishimba - ashukuru hakutua kwenye 18 za akina mama shupavu hawa!!!!

Pamoja na yote, kwa kuwa JF ni mtambo ulioenea kwingi duniani, wala sintoshangaa kusikia ama kundi fulani la akinamama wanasheria, akina mama waandishi wa habari au hata NGOs tu zitakua zimefikiwa na gadhabu hizi hizi zilizotushika humu na pengine kesho tukasikia kwamba huyo Odol na fedha zake zote anahenyeshwa lupango.

Ama kweli unyama kama huu katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia kweli!!!!!!!!!!!!!

Uliyoyanena yana ukweli sipingi lakini kumbuka kuna wakina mama nao wanawapa kibano kama iko upande wa waume zao pia isitoshe huyu jamaa hakumtendea haki huyp dada lakini nazidi kujiuliza chanzo nini mpaka wakafikia hapo
Jioni njema wana Beijing wote
 
Mkuu tuko pamoja kwa kuweka wazi kwamba siku hizi hata mi-dume nao hula kibano nyuma ya milango ya nyumba zao lakini kwa sasa macho ya Afrika Mashariki mote ni kwa ukatili wa huyu Oduol kwa mwana mama huyu.
 
Back
Top Bottom