William Ruto aunda chama chake kipya cha siasa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu Kenya 2022

William Ruto aunda chama chake kipya cha siasa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu Kenya 2022

game over

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2016
Posts
10,727
Reaction score
24,840
Baada ya kutoelewana kwa muda Mrefu kati ya Rais wa Kenya Uhuru Kenya na Makamu wake Wiliam Ruto hali iliyotokana na uhuru kuonesha wazi wazi kutomuunga mkono Ruto kujinyakulia urais 2022 na badala yake kuungana na RAO wa Upinzani kupitia Handshake, (Hand cheque) na BBI.

sasa Bwana Ruto ameona kama Mbwai na iwe Mbwai, Mambo yasiwe mengi, ameamua kujitenga na kuendeleza Hustler Movement kivyake kwa Kuanzisha Chama Kipya, (United Democratic Aliance-UDA).

Ikumbukwe Bila ya Ruto Uhuru asingekuwa Rais wa Kenya. Kwa Sasa Ruto ni ameshajilimbikizia pesa nyingi ambayo itamfanya afadhili kampeni zake na shughuli mbalimbali za Chama chake Kipya ikiwemo Hustler na Wheelbarrow movements.

William Ruto ameonesha wazi kutounga mkono BBI, (BBI Nonsense kama Wakenya wanavyosema)

Ikumbukwe kila awanu ya uchaguzi nchini Kenya Vyama vipya huzaliwa na Kufa awamu inayofuatia.

Tangu Kenya imepata uhuru ni Wakikuyu na Wakelenjini pekee ndio wameiongoza kwa nafasi za juu. Wiliam Ruto pia anatoka kabila hilo na kwa Ukubwa wa kabila lake basi ni wazi ana nafasi kubwa ya kuwa Rais wa Kenya, hii ni kwa sababu Kenya uchaguzi hufanyika kwa misingi ya Kikabila.

CCM ndio chama pekee chenye uzoefu na utulivu ukanda huu, ni muda sasa kaka Mkubwa kuwapa darasa hawa Wakenya namna gani ya kucheza figisu pasi ya kumwaga damu au kuunda vyama vipya kila uchao.
Tatizo watanzania hawajielewi tu.
 
CCM ndio chama pekee chenye uzoefu na utulivu ukanda huu, ni muda sasa kaka Mkubwa kuwapa darasa hawa Wakenya namna gani ya kucheza figisu pasi ya kumwaga damu au kuunda vyama vipya kila uchao.
Ila CCM kwa figisu, fitna na kufunika kombe ili mwanaharam apite, sidhani Afrika kuna nchi inawafikia.
 
Ila CCM kwa figisu, fitna na kufunika kombe ili mwanaharam apite, sidhani Afrika kuna nchi inawafikia.
Itachukua muda sana Upinzani wa Tz Kusimama na Kutunishiana Misuli na ccm.. Maana Wakitaka kusimama tu wanapenyezewa kina Lowasa, Sumaye na Ben Membe wanarudi kwenye Square one.
 
Itachukua muda sana Upinzani wa Tz Kusimama na Kutunishiana Misuli na ccm.. Maana Wakitaka kusimama tu wanapenyezewa kina Lowasa, Sumaye na Ben Membe wanarudi kwenye Square one.
CCM kwa mazingaombwe acha tuu, ni hodari sana wa kusuka na kufumua, kutwanga na kupepeta. Wanaweza kukutengenezea muvi dunia nzima ikadhani ni ya "action" kumbe ni "romance" tu.
 
CCM kwa mazingaombwe acha tuu, ni hodari sana wa kusuka na kufumua, kutwanga na kupepeta. Wanaweza kukutengenezea muvi dunia nzima ikadhani ni ya "action" kumbe ni "romance" tu.
[emoji3][emoji3][emoji3] movie ya x dunia inazani ni movie ya action.
 
Ila Kenya ni nchi ya kipuuzi sana.. Sidhani kama nitawahi kwenda huko kenya
Unaenda tu mzee, ukiachana na siasa, ubaguzi na roho mbaya, kuna some Vibe pia kitaa. Na kama una biashara zako Kenya ni bonge la soko.
 
CCM kwa mazingaombwe acha tuu, ni hodari sana wa kusuka na kufumua, kutwanga na kupepeta. Wanaweza kukutengenezea muvi dunia nzima ikadhani ni ya "action" kumbe ni "romance" tuu.
Weee Jamaa ni nyoko kweli...
 
Back
Top Bottom