William Ruto aunda chama chake kipya cha siasa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu Kenya 2022

William Ruto aunda chama chake kipya cha siasa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu Kenya 2022

Ccm washukuru wananchi wa Tanzania Ni WAVUMILIVU.
Ila sio Kama wanakubalika
CCM ndio chama pekee chenye uzoefu na utulivu ukanda huu, ni muda sasa kaka Mkubwa kuwapa darasa hawa Wakenya namna gani ya kucheza figisu pasi ya kumwaga damu au kuunda vyama vipya kila uchao.
 
Baada ya kutoelewana kwa muda Mrefu kati ya Rais wa Kenya Uhuru Kenya na Makamu wake Wiliam Ruto hali iliyotokana na uhuru kuonesha wazi wazi kutomuunga mkono Ruto kujinyakulia urais 2022 na badala yake kuungana na RAO wa Upinzani kupitia Handshake, (Hand cheque) na BBI.

sasa Bwana Ruto ameona kama Mbwai na iwe Mbwai, Mambo yasiwe mengi, ameamua kujitenga na kuendeleza Hustler Movement kivyake kwa Kuanzisha Chama Kipya, (United Democratic Aliance-UDA).

Ikumbukwe Bila ya Ruto Uhuru asingekuwa Rais wa Kenya. Kwa Sasa Ruto ni ameshajilimbikizia pesa nyingi ambayo itamfanya afadhili kampeni zake na shughuli mbalimbali za Chama chake Kipya ikiwemo Hustler na Wheelbarrow movements.

William Ruto ameonesha wazi kutounga mkono BBI, (BBI Nonsense kama Wakenya wanavyosema)

Ikumbukwe kila awanu ya uchaguzi nchini Kenya Vyama vipya huzaliwa na Kufa awamu inayofuatia.

Tangu Kenya imepata uhuru ni Wakikuyu na Wakelenjini pekee ndio wameiongoza kwa nafasi za juu. Wiliam Ruto pia anatoka kabila hilo na kwa Ukubwa wa kabila lake basi ni wazi ana nafasi kubwa ya kuwa Rais wa Kenya, hii ni kwa sababu Kenya uchaguzi hufanyika kwa misingi ya Kikabila.



Lazima UDA litazoa watu nyomi.
😆😁😀
 
Politics za kenya hazijawa institutionalized zipo Tribalized ndio maana mtu haangalii ideology wala manifesto za Chama fulani, wao ni kabila tu basi, Tanzania hata mtu akubalike vipi hawezi kuwa mkubwa zaidi ya Chama
Inashangaza baadhi ya watu wanasemaga wanataka taasisi zenye nguvu wakati taasisi (CCM) teyari ipo mbele ya macho yao.

Naukiangalia utendaji wa CCM unaona unafanana na ule wa chama cha kikomunisti cha China, yaani hakuna aliye juu ya chama. Hata kama unapesa, ukikosea unanyongwa tuu.
 
Inashangaza baadhi ya watu wanasemaga wanataka taasisi zenye nguvu wakati taasisi (CCM) teyari ipo mbele ya macho yao.

Naukiangalia utendaji wa CCM unaona unafanana na ule wa chama cha kikomunisti cha China, yaani hakuna aliye juu ya chama. Hata kama unapesa, ukikosea unanyongwa tuu.
Kwnz ndani ya CCM kuna demokrasia kubwa sn, nani alijua mtu km Magufuli ambaye hakuwa na nguvu yyte ndani ya chama angeiwakilisha CCM ktk kinyang'anyiro cha urais.
 
Back
Top Bottom