Ambiente Guru
JF-Expert Member
- May 21, 2012
- 2,605
- 1,085
Wao wana rasilimali za kuiba kwani?
Nakubaliana na hoja iliyoko hapo kwenye red japo sikubaliani na hoja za Rais wa Senegal ambazo Ruto amezitumia kama rejea. Rais wa Senegal "amejitetea" mbele ya Obama kwamba hawezi kuruhusu "haki za mashoga" just because Senegal ina "waislamu wengi". Utetezi mfu kabisa kwa Rais wa nchi.
Umemaliza.na hivi ndivyo ilivyo na ndivyo Obama alivyosema.hawa ni watuhumiwa wa ICC,msidanganyike eti hawamind wee!!kasema nani???wakenya nchi nzima hawakwenda kazini kusherehekea ushindi wa Obama awamu ya kwanza halafu wasikie mtoto wao anatembelea nyumba ya jirani na kwao hataki kwenda,hata wewe ingekuuma tu wana wakati mgumu ila kikombe hicho hawawezi kukikwepa.Mkuu wakati anaahidi kutembelea Kenya walikuwa hawajawachagua hawa washtakiwa wa ICC! .
Sababu kubwa iliyomfanya asitembelee Kenya ni kutokana na kesi inayowakabili Raisi na Makamu wake ICC.
hao akina ruto wanajiliwaza bure na kutaka kenyans wasione kama ni issue obana ku-skip nchi yao. Kwani hawajui kuwa wao ndo kikwazo cha obama kutokwenda kenya??
Kumbe kutembelewa na Obama ni ujiko? Sikujua hilo, Kama walinzi wake tu wana fanya sorting ya mawaziri and other gorvernment officials wa kwenda kumsalimu, ni dhihaka kiasi gani hiyo? Mzee mchonga aliisha wahi mpa kifimbo chake Malkia Elizabeth!
Kumbe kutembelewa na Obama ni ujiko? Sikujua hilo, Kama walinzi wake tu wana fanya sorting ya mawaziri and other gorvernment officials wa kwenda kumsalimu, ni dhihaka kiasi gani hiyo? Mzee mchonga aliisha wahi mpa kifimbo chake Malkia Elizabeth!
Obama atatembelea akimaliza uongozi wake kama mtu mwenye asili ya Kenya na sio sasa... kwa sasa wamalizane na ICC kwanza... uraisi wa marekani ni taasisi sio matakwa ya obama... USA stands against violency and it will contradict if he visits now... well done Obama...
WanaJF!
Nimekuwa nikiwaza mahusiano ya Tanzania na nchi jirani za Afrika ya mashariki baada ya ujio wa Obama yatakuwaje?
Kwani inasemekana kitendo cha Obama kuja Tanzania na kuiruka Kenya, kimeleta gumzo, sio tu ndani ya Kenya, bali hata mataifa mengine yameshangazwa na kitendo hicho. Kwani ukizingatia asili ya rais Obama na ahadi yake kwa Kenya, ni wazi kwamba alipaswa atembelee na Kenya kama sehemu ya ziara yake hapa Afrika mashariki.
Sitakuwa na mengi ya binafsi juu ya hili la Ruto na dhihaka yake kwa ujio wa Obama Afrika, bali nime ambatanisha maelezo yake mwenyewe kama ifuatavyo;
NAIBU wa Rais Bw William Ruto, jana alivunja kimya chake kuhusu hatua ya rais wa Marekani Barack Obama kutozuru nchini Kenya kwa kusema hatua hiyo haina madhara yoyote kwa Kenya.
Huku akiongea katika kanisa la Katoliki la St Gabriel Bahati, kaunti ya Nakuru, Bw Ruto alisema "nchi hii ina 'marafiki wengine wengi duniani ambao inaweza kushirikiana nao huku akiongezea kuwa hatua ya rais Obama kukwepa kutembelea Kenya haiwezi kutatiza kwa vyovyote vile uhusiano mwema uliopo wa kibiashara baina ya Marekani na Kenya."
Bwana Ruto akasema, Tunaiheshimu nchi ya Marekani nayo inafaa kuwaheshimu Wakenya,
Alisema serikali ya Kenya tayari imeanzisha mikakati ya kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na mataifa mengine huku akikariri kuwa safari ya Rais Uhuru Kenyatta nchini Uganda ambapo alikutana na rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni na mwenzao wa Rwanda rais Paul Kagame kujadili jinsi nchi hizo tatu zinaweza kushirikiana kibiashara, ni miongoni mwa mikakati hiyo.
Pia akaongezea, Nchi yetu inamcha Mungu na kamwe hatutaruhusu mataifa ya kigeni kutuletea tamaduni ambazo zinakinzana na desturi zetu, akasema Bw Ruto huku akirejea hotuba ya Rais Obama nchini Senegal ambapo aliitaka nchi hiyo kuheshimu haki za Mashoga."
Kenya wana wivu wa kijinga sana, nilikuwa naangalia TV moja ya kenya leo asubuhi imenishangaza sana sikujua kama hiliswala la Obama kuja Tanzania limewaathiri kwa kiasi kikubwa hivyo. mtangazaji mmoja akasema "Obama angekuja Kenya akae hata masaa mawili", mwingine akasema "hata bila US kenya itaendelea tu na inazidi kusonga mbele." Yaani Wakenya wamekuwa very desperate, wanatamani hata kulia. Huku Watanzania wengi wanaona hiyo ni ishu ya kawaida sana kutembelewa na marais wa US ambao huja kuzoa utajiri wetu.
Udhalilishaji waliotufanyia hawa Marekani wa kutupangia mpaka mawaziri wa kwenda kuonana na Obama, usingefanyika enzi ya utawala wa "MUSSA"!!
naona umeongea kiingereza inaonyesha kama msomi au ndo wale wa shule za english medium lakini kichwani hakuna.Hoja ya kimsingi hapa fedha iliyotolewa kwenye miradi ya umeme ikasimamiwa ipasavyo , je tutabaki kama mwanzo na upungufu wa umeme?hizo ni fedha tumepewa misaada ni wajibu wetu sasa kusimamia kuleta maendeleo , ni hatua kuliko hapo awali.jamani tuwe wachambuzi wa kila kitu kulaumu, kubeza, kudharau, pale kwenye hatua ya maendeleo lazima tusema na tupongeze maana pesa ni pesa hata kama imetokea chooni , ina msaada kwenye hatua ya kutatua hoja za manunuzi.Mradi huo wa umeme ni nchi nyingi wanautaka na hawajapa, hivyo mdau jipongeze kuona kuwa nasi hata kama ni watu wa mikataba mibovu , lakini pesa tumepewa itusaidie.Ni wajibu wa bunge letu kuisimamia serikali utekelezeke ipasavyo na si kubweteka baadaye kuja na malalamiko.Aende asiende what difference does it make?Stupid Africans.