Kumekuwapo na Taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, hususani Facebook kupitia ukurasa wa Mjumbe Plus, likidai kuwa William Ruto ametoa kauli akiwapongeza Watanzania kwa kuwa na Rais mcha Mungu na mpenda haki.
Chapisho hilo linaambatana na ujumbe unaosomeka:
“Watanzania, katika jambo ambalo mnapaswa kufanya ni kumheshimu Rais Samia, maana ndiye Rais anayewapenda raia wake katika shida na raha, na pia ana hofu ya Mungu ndani yake. Hayuko tayari kuona raia wake wanateseka hata kidogo kwa sababu ya ukandamizaji wa haki. Mimi nawaomba mumpende Rais wenu, kwani hamtajutia kamwe.” Rais wa Kenya, William Ruto
Uhalisia ni upi?
Ufuatiliaji wa kimtandao kupitia nyenzo za kidigitali hakuna chanzo rasmi kilichomnukuu William Ruto akitoa kauli hiyo. Aidha, uchunguzi tovuti na kurasa rasmi za mawasiliano za serikali ya Kenya, hakuna kumbukumbu yoyote inayoonyesha Rais huyo kama aliwahi kutoa ujumbe huo unaosambazwa mtandaoni.
Aidha Rais Ruto alizungumza kuhusu uchaguzi wa Tanzania wakati wa mahojiano na chombo cha habari cha kimataifa cha
Al Jazeera. Katika mahojiano hayo alisisitiza kuwa kila nchi ina mfumo wake wa kushughulikia masuala ya uchaguzi, akisema si jukumu lake kuhukumu Tanzania. Alieleza kuwa katika demokrasia ya ushindani, matokeo ya ushindi mkubwa sana (kama zaidi ya asilimia 90) si ya kawaida katika nchi kama Kenya.
Vilevile, baada ya uchaguzi,
alitoa pongezi kwa Samia Suluhu Hassan na kuhimiza amani, uvumilivu na mazungumzo ya kisiasa, bila kutumia maneno ya kumsifu kwa mtindo unaodaiwa kwenye chapisho hilo.
Hivyo ujumbe huo unaosambaa mtandaoni si kauli rasmi ya Rais wa Kenya.