Ni kweli lakini siyo kwa utitiri kama huu tulio nao, Leo hii nikiweke sentensi moja ya kiswahili nikawaita watu sita wa lugha tofauti kila mtu aitafsiri kwenye lugha yake utapata mkanganyo wa ajabu sana.
Pamoja na Mapungufu yao tuwapongeze ndugu zetu Waislamu kwenye kudhibiti lugha imewasaidia sana ndo maana kwao unaona wapotoshaji ni wachache sana ukilingana na sisi wakristo.
Ukijaribu kuangalia baada ya Yesu kuondoka kanisa la kwanza liliendelea kupanua huduma zake pande nyingi za Dunia na ivyo wahubiri au tuseme wainjilishaji wapya walianza kuwepo lakini kwa kukwepa kusije kuwepo upotoshaji walibaki kuwa na centre moja Pale Jerusalem kwa akina petro, mambo yakijitokeza huko wanakuja kuuliza pale: mfano Paulo na kisa cha kutahiri, lakini kwa sasa hamna Centre kama hizi kila mtu ni mjuaji anafanya inavyomfaa, angalau tungekuwa standard moja ingesaidia.
Sent from my TECNO-L8 using
JamiiForums mobile app