William Tyndale alichomwa moto mpaka kufariki kwa kutafasiri Biblia kutoka kwenye lugha ya Kigiriki kuiingiza kwenye kingereza

William Tyndale alichomwa moto mpaka kufariki kwa kutafasiri Biblia kutoka kwenye lugha ya Kigiriki kuiingiza kwenye kingereza

Ni kweli lakini siyo kwa utitiri kama huu tulio nao, Leo hii nikiweke sentensi moja ya kiswahili nikawaita watu sita wa lugha tofauti kila mtu aitafsiri kwenye lugha yake utapata mkanganyo wa ajabu sana.
Pamoja na Mapungufu yao tuwapongeze ndugu zetu Waislamu kwenye kudhibiti lugha imewasaidia sana ndo maana kwao unaona wapotoshaji ni wachache sana ukilingana na sisi wakristo.

Ukijaribu kuangalia baada ya Yesu kuondoka kanisa la kwanza liliendelea kupanua huduma zake pande nyingi za Dunia na ivyo wahubiri au tuseme wainjilishaji wapya walianza kuwepo lakini kwa kukwepa kusije kuwepo upotoshaji walibaki kuwa na centre moja Pale Jerusalem kwa akina petro, mambo yakijitokeza huko wanakuja kuuliza pale: mfano Paulo na kisa cha kutahiri, lakini kwa sasa hamna Centre kama hizi kila mtu ni mjuaji anafanya inavyomfaa, angalau tungekuwa standard moja ingesaidia.

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
Kiukweli KWA logic ya kawaida maneno haya yana make sense kama ulivyosema huenda pia ulikuwa ni mpango wa MUNGU au wa shetani vyote vinawezekana. Mimi nakubali hii kitu inasababisha kuwepo na denominations nyingi ndani ya ukristo
 
Uuaji kwa wenyewe ni jambo baya.

Msimamo wa Kanisa Katoliki juu ya imani ikiwa ni pamoja na kutafsiri biblia ni mambo yanayochukuliwa kwa uangalifu mkubwa.

Tunafahamu kwamba lugha ni chombo cha mawasiliano pia kufundishia na kujifunzia mafundisho.

Jambo moja wazi kuhusu lugha ni kwamba lugha inayotafsiriwa inaweza kwa wakati huo isijitosheleze na hivyo kupotosha mafundisho.

Kumbe kinachohitajika si tafsiri lakini jamii ina uelewa wa kina wa mambo na elimu ya vitu hivi kwamba mapungufu katika lugha inayotafsiriwa hayawezi kupotosha ukweli.

Kama mtu kwa tafsiri yake anaharibu ukweli hivi kwamba anahatarisha maisha ya watu kiroho na kimwili, unafikiri busara hapo ni nini?

Mimi sipendekezi uuaji lakini nini unafikiri mamlaka inayohusika ikishajidhihirisha kuwa jambo hilo linaleta madhara makubwa kwa ukweli itachukuwa hatua gani.
 
Back
Top Bottom