Salaam Wadau wa Michezo,
Kuna taarifa nimeiona inadai kuwa Willy Esomba Onana aliyekuwa mchezaji wa Simba SC msimu uliopita ameibuka shujaa kwa kufunga mabao matatu katika mchezo wake wa kwanza wa kirafiki. Taarifa hiyo nimeiona kwenye akaunti ya Instagram ya Aggy Simba na kwa SeekerTZ.
Kuna taarifa nimeiona inadai kuwa Willy Esomba Onana aliyekuwa mchezaji wa Simba SC msimu uliopita ameibuka shujaa kwa kufunga mabao matatu katika mchezo wake wa kwanza wa kirafiki. Taarifa hiyo nimeiona kwenye akaunti ya Instagram ya Aggy Simba na kwa SeekerTZ.
- Tunachokijua
- Leandre Willy Essomba Onana (amezaliwa 14 Julai 2000) ni mchezaji maarufu wa soka kutoka Cameroon, anacheza nafasi ya kiungo wa kati. Kabla ya kujiunga na Simba S.C. tarehe 1 Julai 2023, Onana alikuwa mchezaji wa klabu ya Rayon Sports nchini Rwanda katika msimu wa 2022-2023, ambapo alifunga magoli 16 katika mechi 23 alizocheza.
Kwa sasa, anacheza katika klabu ya Al Hilal Benghazi ya Libya, baada ya kujiunga nao mnamo Agosti 20, 2024 akitokea Simba S.C. ya Tanzania.
Kumekuwa taarifa zinadai kuwa baada ya Onana kusajiliwa Al Hilal Benghaz ameteka vichwa vya habari na mioyo ya Mashabiki wa timu hiyo mpya baada ya kufunga magoli matatu kwenye mechi yake ya kwanza.
Je kuna ukweli kuhusu taarifa hiyo?
JamiiCheck imefanya ufuatiliji wa kimtandao kwa kupitia Live Score, Sofa Score ambazo zinaonesha timu ya Al Hilal Benghaz imecheza michezo miwili tu tangu Onana ajiunge nayo Agosti 20, 2024.
Mechi mbili za Al Hilal Benghaz tangu Onana ajiunge Agost 20, 2024
Mechi ya kwanza ilikuwa Agosti 23, 2024 ambapo Al Hilal Benghaz ilikuwa ya mkondo wa pili wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Kitara FC na Hilal iliibika na magoli 3-2 huku magoli hyo yakifungwa na Mohamed Salim na mengine mawili yakifungwa na Hemeya Tanjy.Vyanzo vinaonesha kuwa Onana hakucheza mcheo huo.
Takwimu za Mechi ya Al Hilal Benghaz na Kitara pamoja na majina ya waliofunga. Jina la Onana halipo
Vyanzo, hivyo vinaonesha kuwa mchezo wa pili wa Al Hilal Bengaz tangu Onana asajiliwe ulikuwa ni wa Kirafiki ambao timu hiyo ilicheza dhidi ya Club Africein ya Tunisia uliochezwa Septemba 9, 2024.
Mchezo huo ndiyo umekuwa mechi ya kwanza Onana kucheza na yeye tangu kuchapisha picha kwenye Ukurasa wake wa Instagram huku caption ikiandikwa kwa kiingereza Friendly game na emoj ya mipira mitatu huku watu wakitafsiri kama kafunga Hatrick (tazama hapa).
Chapisho la Onana kwenye ukurasa wake wa Instagram baada ya mechi
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa Matokeo ya Mchezo huo yalikuwa ni sare ya goli 1-1 huku goli la Hilal likifungwa na Hemed El Thalba huku la Club Africain likifungwa na Bilel Ait Malek.
Mpaka sasa hakuna chanzo chochote kinachoonesha kuwa Onana ameshafanikiwa kupata goli lolote tangu ajiunge na timu yake hiyo baada ya kuondoka Simba.
Takwimu za mcheo wa kirafiki kati ya Al Hilal Bengaz dhidi ya Club Africain