Wimbi jipya linaendelea kufanya yake na pengine hatuoni hadi likishapita

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,478
Reaction score
3,659
Kuna wimbi jipya na linapita kwa kasi sana. Ndani ya hilo wimbi yapo tunayoyajua lakini yapo ambayo hatuyajui ama tunayahisi, na wakati ukifika ndio tutajua kama tulikuwa hatujui. Audha kama hatutakuwepo, watakaokuja ndio wataona kwa uwazi zaidi maana walikuwa nje ya wimbi. Nao wataishi katika maisha ambayo wimbi limefanya. Huwa nina msemo wangu; kwamba think before nature. Kwamba chukulia mvua imenyesha kubwa ikatengeneza mafuriko. Mafuriko yakala nyumba yako na vilivyomo. Baada ya mafuriko inakulazimu kuanza maisha mapya au ujenzi upya, au kuhama kabisa kwa lengo la kuepuka dhahama nyingine. Kiufupi hutakuwa yue wa awali. Utaishi kwa tahadhari zaidi.

Wakati siasa iko constant, dini na maadili viko dynamic, tena to the wrong direction. Nitaanza na dini. Dini hasa ukristo unapata wakati mgumu sana kwa wakati huu. Pengine kwa kuwa katika ukristo kuna uhuru na demokrasia sana ndio maana yapo mengi yanaendelea. Waumini kwa kasi sana wanahoji masuala ya kiimani na mitazamo ya madhehebu yao. Ni kama vile walikuwa wamelala au wanasubiri wakati fulani ufike. Imani inaanza kuhojiwa sana. Wakati mwingine hata sisi waumini ambao hatutetereki kiimani kwa maana ya kuyumbishwa na na kelele nyingi za hawa wanaojiita mitume na manabii, tunapata mashaka juu ya kile tunachokiamini. Maana kama ni msomaji wa biblia utagundua kuwa mambo mengi yafanywayo sasa yalishazungumziwa na mitume. Mengi yamezungumzwa na mitume kuanzia amatendo ya Mitume hadi kitabu cha Yuda. Hapo hujagusa mafundisha ya Yesu.

Ndipo wakati fulani nikakutana na andiko toka 2 Timotheo 4:3-4 linasema Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundiso yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo. Neno la Bwana. Katika mkumbo huu si waumini tu bali hata hao wanaojiita mitume na manabii nao wameanza kuchanganya habari. Mara utasikia Yesu si Mungu, utasikia suala la kuoa mke mmoja ni siasa za enzi za Rumi, mara heri waislam katika hili na lle (nao wana vimeo vyao vingi tu sema hawasemeki hawa 😉). Ni mwendo wa dhehebu kurushiana michanga na dhehebu lingine huku waumini wakiendelea kugawanyika na kusambaratika.

Ukiangalia msingi wa madhehebu mengi hapa nchini na duniani ni Kanisa Katoliki. kwa kanisa hili kuwa katika misimamo ya kimapokeo na kiutamadunisho, wale wanaoona aidha hawawezi kusimama na taratibu hizo, au wanaona wamefunuliwa sana upeo wa kimungu ndio huchomoka na kwenda kuanzisha naviita vidhehebu, na kwa bahati mbaya hupata waumini. Waliobaki waumini katika ukatoliki, wapo wengi pia ambao huendelea kuhoji taratibu kadha wa kadha za kikanisa na kiliturujia ila bado wakaendelea kuwepo kwa kuwa tu tayari wapo ndani ya mfumo.

Hapa nataka nisemee huu mfumo. Kila taasisi ya kidini huwa inajiwekea mfumo wake. Naamini sana kuwa mfumo wa kiimani wa kanisa Katoliki uko vizuri. Nazungumzia Katoliki maana nami ni Mkatoliki. Siku zinavyokwenda, mfumo huu unazidi kupata misukosuko toka kwa watu wenye nia zao wanaozijua wenyewe. Mfumo wa kanisa, na mifumo ya madhehebu mengine lengo lake ni kuona kuwa mwanadamu anaishi kinidhamu. Pasingekuwepo na hii nidhamu basi dunia ingekuwa chafu sana. Kwa bahati mbaya ndiko inakoelekea kama taasisi hizi za kidini pamoja na mafundisho yao hawatakuwa makini kujua namna ya kuishi na waumini wao.

Dunia bila dini wala hofu ya Mungu ni jehanamu. Katika hili wapo watu ambao wanaujua ukweli na wana uwezo wa kuishi bila dini na wakazifuata njia zilizo sahihi kabisa. Wengi wetu bila dini na imani hatuwezi kutawalika. Viongozi wa dini wanajua. Wana siri zao mioyoni kuhusu maisha haya ya kiimani. Ni kama vila wanajua ilipo pini ya kufyatulia bomu, halafu kuna kundi kubwa la watu linaitafuta hiyo pini ila hawaelezwi ilipo kwa kuwa wataleta shida sana. Kikubwa kinachowakimbiza waumini huko makanisani ni MICHANGO. Hivyoili kuleta mshikamano na kuishi katika mfumo/mifumo, makanisa yetu yatazame hili suala. Michango isije kuwa sababu ya waumini kuishi maisha wanayotaka. Kukimbia na kuhama makanisa na hatimaye kuwa wapagani. Ulaya makanisa mengi yameshafungwa. Afrika huku viongozi wa kidini nanyi msiwe sababu ya kuwabughudhi waumini kiasi cha kutangatanga na kupoteza mwelekeo wa kiimani. Waumini wengi hawajaandaliwa kuishi nje ya mifumo ya kiimai, hivyo mtasababisha mtafaruku mkubwa sana wa jamii ambayo mmeweza kuimudu kwa kitambo kirefu na sasa ni kama zizi lililofunguliwa na kondoo wanatawanyika ambapo kuwarudisha ni ngumu sana.

Tuishie hapa kwa leo.
 
Nikurekebishe kidogo tu mkuu , viongozi wengi wa dini hawajui lolote ni fuata mkumbo tu niamini mimi.
 
Tapeli Kwa mgongo wa dini.Kamateni hao hao nyumbu ndio muwafanye hivi 👇
Screenshot_20240612-185652.jpg
 
Viongozi wamewachia mhangaike na manabii na mitume huku wao wakila bata kwa mrija kwani hamwasumbui.
Si manabii na mitume tu, wamewaongezea visungura na viroba mpaka kwenye maduka ya wapemba, mmepewa bonasi ya uchambuzi wa mpira kutwa nzima na kubeti kila mahali.
 
Uwanja wa mbagara zakhemu ukipita pale mida ya saa 1 usiku utakuta vijana wameweka vikundi vikundi wakijadiriana Mambo. Siku nami nikaenda kusikiriza wanacho ongea hee Eti wanajadiri Simba na yanga😄😄😄😄 yani watu mpaka mishipa ya shingo imesimama.
 
Ndio sio kitabu kibaya moja kwa moja , kwa nini unafikiri hivi?
Min
Usiue, usizini, heshimu wazazi wako, usiseme uongo, usitamani mke wa jirani yako na mengine mengi ambayo hata katika mzani wa kimantiki ni mazuri na yanaweza kuchambuliwa.

Nilkuwa nasubiri ulisema nipo tayari kuutafuta ukweli, na ni kwa engo gani viongozi wa dini hawajui lolote na niwafata mkumbo?
 
Vyote hivyo unaweza kuvifuata toka ndani yako ukijitambua tu ,utu na upendo sio kitu cha kufundishwa ukiwa nacho ndani yako.
 
Kuna wimbi jipya na linapita kwa kasi sana. Ndani ya hilo wimbi yapo tunayoyajua lakini yapo ambayo hatuyajui ama tunayahisi, na wakati ukifika ndio tutajua kama tulikuwa hatujui. Audha kama hatutakuwepo, watakaokuja ndio wataona kwa uwazi zaidi maana walikuwa nje ya wimbi. Nao wataishi katika maisha ambayo wimbi limefanya. Huwa nina msemo wangu; kwamba think before nature. Kwamba chukulia mvua imenyesha kubwa ikatengeneza mafuriko. Mafuriko yakala nyumba yako na vilivyomo. Baada ya mafuriko inakulazimu kuanza maisha mapya au ujenzi upya, au kuhama kabisa kwa lengo la kuepuka dhahama nyingine. Kiufupi hutakuwa yue wa awali. Utaishi kwa tahadhari zaidi.

Wakati siasa iko constant, dini na maadili viko dynamic, tena to the wrong direction. Nitaanza na dini. Dini hasa ukristo unapata wakati mgumu sana kwa wakati huu. Pengine kwa kuwa katika ukristo kuna uhuru na demokrasia sana ndio maana yapo mengi yanaendelea. Waumini kwa kasi sana wanahoji masuala ya kiimani na mitazamo ya madhehebu yao. Ni kama vile walikuwa wamelala au wanasubiri wakati fulani ufike. Imani inaanza kuhojiwa sana. Wakati mwingine hata sisi waumini ambao hatutetereki kiimani kwa maana ya kuyumbishwa na na kelele nyingi za hawa wanaojiita mitume na manabii, tunapata mashaka juu ya kile tunachokiamini. Maana kama ni msomaji wa biblia utagundua kuwa mambo mengi yafanywayo sasa yalishazungumziwa na mitume. Mengi yamezungumzwa na mitume kuanzia amatendo ya Mitume hadi kitabu cha Yuda. Hapo hujagusa mafundisha ya Yesu.

Ndipo wakati fulani nikakutana na andiko toka 2 Timotheo 4:3-4 linasema Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundiso yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti; nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo. Neno la Bwana. Katika mkumbo huu si waumini tu bali hata hao wanaojiita mitume na manabii nao wameanza kuchanganya habari. Mara utasikia Yesu si Mungu, utasikia suala la kuoa mke mmoja ni siasa za enzi za Rumi, mara heri waislam katika hili na lle (nao wana vimeo vyao vingi tu sema hawasemeki hawa 😉). Ni mwendo wa dhehebu kurushiana michanga na dhehebu lingine huku waumini wakiendelea kugawanyika na kusambaratika.

Ukiangalia msingi wa madhehebu mengi hapa nchini na duniani ni Kanisa Katoliki. kwa kanisa hili kuwa katika misimamo ya kimapokeo na kiutamadunisho, wale wanaoona aidha hawawezi kusimama na taratibu hizo, au wanaona wamefunuliwa sana upeo wa kimungu ndio huchomoka na kwenda kuanzisha naviita vidhehebu, na kwa bahati mbaya hupata waumini. Waliobaki waumini katika ukatoliki, wapo wengi pia ambao huendelea kuhoji taratibu kadha wa kadha za kikanisa na kiliturujia ila bado wakaendelea kuwepo kwa kuwa tu tayari wapo ndani ya mfumo.

Hapa nataka nisemee huu mfumo. Kila taasisi ya kidini huwa inajiwekea mfumo wake. Naamini sana kuwa mfumo wa kiimani wa kanisa Katoliki uko vizuri. Nazungumzia Katoliki maana nami ni Mkatoliki. Siku zinavyokwenda, mfumo huu unazidi kupata misukosuko toka kwa watu wenye nia zao wanaozijua wenyewe. Mfumo wa kanisa, na mifumo ya madhehebu mengine lengo lake ni kuona kuwa mwanadamu anaishi kinidhamu. Pasingekuwepo na hii nidhamu basi dunia ingekuwa chafu sana. Kwa bahati mbaya ndiko inakoelekea kama taasisi hizi za kidini pamoja na mafundisho yao hawatakuwa makini kujua namna ya kuishi na waumini wao.

Dunia bila dini wala hofu ya Mungu ni jehanamu. Katika hili wapo watu ambao wanaujua ukweli na wana uwezo wa kuishi bila dini na wakazifuata njia zilizo sahihi kabisa. Wengi wetu bila dini na imani hatuwezi kutawalika. Viongozi wa dini wanajua. Wana siri zao mioyoni kuhusu maisha haya ya kiimani. Ni kama vila wanajua ilipo pini ya kufyatulia bomu, halafu kuna kundi kubwa la watu linaitafuta hiyo pini ila hawaelezwi ilipo kwa kuwa wataleta shida sana. Kikubwa kinachowakimbiza waumini huko makanisani ni MICHANGO. Hivyoili kuleta mshikamano na kuishi katika mfumo/mifumo, makanisa yetu yatazame hili suala. Michango isije kuwa sababu ya waumini kuishi maisha wanayotaka. Kukimbia na kuhama makanisa na hatimaye kuwa wapagani. Ulaya makanisa mengi yameshafungwa. Afrika huku viongozi wa kidini nanyi msiwe sababu ya kuwabughudhi waumini kiasi cha kutangatanga na kupoteza mwelekeo wa kiimani. Waumini wengi hawajaandaliwa kuishi nje ya mifumo ya kiimai, hivyo mtasababisha mtafaruku mkubwa sana wa jamii ambayo mmeweza kuimudu kwa kitambo kirefu na sasa ni kama zizi lililofunguliwa na kondoo wanatawanyika ambapo kuwarudisha ni ngumu sana.

Tuishie hapa kwa leo.
Hata ungeendelea kuandika anaye tetereka ni mtu na si neno la Mungu. Acha kuheshimu sanamu kwanza. Unavyoviita vidhehenu hawachongi sanamu halafu wakaitembeza nyumba kwa nyumba na kuipa heshima. Wala hawamtumii Mariam kama mwombezi.
 
Back
Top Bottom