HOJA Wimbi la vituo vya mafuta kuunganishwa na biashara nyingine, usalama unazingatiwa ipasavyo?

HOJA Wimbi la vituo vya mafuta kuunganishwa na biashara nyingine, usalama unazingatiwa ipasavyo?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Kwa nyakati tofauti, Serikali imekuwa ikionya kuhusu ujenzi wa vituo vya mafuta katika maeneo ya makazi kwa lengo la kulinda usalama wa wananchi.

Kutokana na uchunguzi niliofanya, nimebaini jambo linaloendelea kwa kasi hivi sasa. Vituo vya mafuta vimekuwa vikiongeza shughuli za kibiashara nje ya uuzaji wa mafuta, zikiwemo, maduka makubwa ya bidhaa (supermarket), karakana za magari, sehemu za kuosha magari na migahawa. Shughuli hizo zinawavutia wananchi wengi kutembelea vituo hivyo kwa huduma mbalimbali hata wasiohusika na uhitaji wa huduma za mafuta.

Hali hiyo imenifanya nijiulize maswali kuhusu usalama wa watumiaji wa vituo hivyo, wafanyakazi na wananchi wanaozunguka maeneo hayo, kutokana na shughuli nyingine zinazofanyika sambamba na uuzaji wa mafuta.

Ingawa biashara hizo zinaweza kuongeza huduma kwa wateja na kukuza uchumi, ni muhimu kubaini kama zinafanyika kwa kuzingatia masharti ya usalama, vibali na mipango ya matumizi ya ardhi iliyoidhinishwa na mamlaka husika. Hatua za kuzuia hatari zinapaswa kuchukuliwa kabla ya majanga kutokea, badala ya kusubiri madhara yatokee ndipo hatua zianze kuchukuliwa.

Katika baadhi ya vituo, kumekuwa na mwingiliano mkubwa wa watu na magari. Hali hiyo inaibua wasiwasi kuhusu idadi ya watu wanaoweza kuathirika endapo kutatokea tukio la ajali au dharura.

Kuongezeka kwa shughuli hizo kunaweza kuongeza mwingiliano wa watu na magari ndani ya maeneo yenye bidhaa zinazoweza kuwaka. Hivyo, ni muhimu kuchunguza namna vituo hivyo vinavyotenganisha maeneo ya biashara, aina za biashara zinazofanyika na sehemu za kuhifadhi, kupakua na kuuza mafuta, pamoja na utayari wake wa kukabiliana na dharura.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na halmashauri, hasa katika Mkoa wa Dar es Salaam, zinapaswa kuhakikisha kunakuwa na usimamizi madhubuti, ukaguzi wa mara kwa mara na utekelezaji wa masharti ya usalama.

Baadhi ya maswali yanayopaswa kufuatiliwa na kujibiwa ili kuipa jamii mrejesho ni pamoja na: Je, shughuli zote zinazofanyika katika vituo hivyo zimeidhinishwa? Ukaguzi hufanyika kwa utaratibu gani, na hatua gani huchukuliwa pale kasoro zinapobainika?

Uchunguzi wa masuala haya ni muhimu ili kubaini kama shughuli hizo zinaendeshwa kwa kuzingatia sheria na viwango vinavyotakiwa, na kuhakikisha hatua za kuzuia hatari zinachukuliwa kabla ya kutokea kwa madhara kwa maisha, mali na mazingira.

Iwapo hakuna utaratibu madhubuti wa kusimamia na kutofautisha shughuli zinazoruhusiwa katika vituo hivyo, kunakuwa na haja ya kuhoji ufanisi wa hatua zinazochukuliwa kuzuia hatari zinazoweza kutokana na matumizi ya maeneo hayo, hasa ikizingatiwa kuwepo kwa marufuku ya Serikali kuhusu vituo hivyo kutotakiwa kujengwa kwenye maeneo ya makazi ya watu.
 
Nimetembea baadh ya nchi, kwenye vituo vya mafuta nakuta mini market,car wash, restaurant

Hivo yaan, kwahiyo sijui watanganyika mnataka nini
 
Ni sawa tu hakuna shida,ni huduma kama huduma zingine,vigezo vya usalama vikizingatiwa.
NB:Mafuta yanawaka hayalipuki ndio maana vituo vipo mtaaani.
 
Pale mwanza kuna kituo cha mafuta kabla hujafika stand ya mabasi ya nyamuhongolo upande wa kulia mwa barabara kama unatoka mjini kuna kituo cha mafuta ndani yake kuna sehemu jioni watu wanakunywa bia halafu kuna jiko limewekwa nje wanachoma na nyama
 
Kuna sheli moja wameweka kibanda cha M-pesa na huduma zingine za kifedha Mobile Money halafu fresh kabisa maishaa yanaendelea vizuri tu
 
Pale mwanza kuna kituo cha mafuta kabla hujafika stand ya mabasi ya nyamuhongolo upande wa kulia mwa barabara kama unatoka mjini kuna kituo cha mafuta ndani yake kuna sehemu jioni watu wanakunywa bia halafu kuna jiko limewekwa nje wanachoma na nyama
Na nyama wanachomea mafuta hayohayo ya sheli.. noma sana pale
 
Kuna vijamaa ofisi za ardhi vinakula rushwa utadhani havina akili nzuri
 
Back
Top Bottom