Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Tanzania ni yetu sote na wewe , denooJ, ukiwemo( vinginevyo useme kabisa hapa kuwa wewe si mtanzania). Kwa hiyo, changamoto zinazomkabili mtanzania wa Songea, Mafinga ,Tanga, Sirali na hata Chakechake tunapaswa kuzitafutia ufumbuzi kwa kila mtanzania kwa nafasi aliyonayo.
Ufumbuzi unaweza kuwa wa kutoa mawazo chanya ama mali ama nguvu kazi kutatua changamoto hiyo. Huo ndiyo muhimili wa roho ya utaifa unaotuleta pamoja kama watanzania. Wasiotutakia mema wako nashughuli nyingi kwa nia ovu ya kuvunja muhimili wetu huu wa utaifa! (Sijasema wewe ni mmojawao).
Kitendo cha baadhi ya watu tena bila aibu kutoka hadharani hasa mitandaoni kushangilia changamoto zinazowakabili wenzetu badala ya kutafuta ufumbuzi, kukebehi juhudi za wanaojaribu kutatua changamoto hizo badala ya kuungana nao kuleta mawazo chanya kupata ufumbuzi nakadhalika nakadhalika, ni kitendo cha ovyo kufanywa na watu tena wanaojinasibu wana akili kubwa!
Nawasihii watanzania wenzangu tuwe na roho ya utaifa na tuionyeshe kwa kuungana pamoja kwa amani na upendo kukabiliana na changamoto zinazotukabili kwa mtanzania mmoja mmoja, kundi ama taifa.
Asanteni kwa kusoma bandiko langu hili.
Hakuna umoja wa kitaifa na majizi ya kura. Anayesababisha haya ni jiwe na approach zake mbovu katika uchumi.