I am Groot
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,929
- 10,747
Nimeona rais Samia akiwa huko ziarani akieleza ni namna gani ameshangazwa na kukuta wamama wazazi (watoto) wodini.
"Nilipokwenda kwenye wodi ya kinamama, na hasa watoto ambao hawajatimia,nimekuta mmoja tu ndio mpevu...lakini wengine wote ni kutoka miaka 15-19, niombe sana, wapeni nafasi watoto wakue kidogo...waacheni waende shule, wapeni nafasi watoto wakue kidogo kuzaa watoto wenzao"Rais Samia
Ni kweli kwa sasa wimbi hili ni kubwa sana na pia ni mzizi wa uwapo wa single mothers wengi hapo mbeleni. Je, ni nani wakulaumiwa? Mabinti wenyewe, wazazi na walezi, Vijana wa rika tofauti huko mitaani, serikali au jamii kwa ujumla?
Ikumbukwe; miaka kadhaa ya nyuma kipindi cha JPM ilitoka amri ya kuwa binti akujifungua akiwa anasoma itakuwa ndio mwisho wa safari yake kielimu. Jambo hili lilipingwa vikali na wanaharakati.
Miaka ya hivi karibuni katika awamu ya sita ya serikali; raisi alitoa tamko kuwa mabinti wakipata ujauzito na kujifungua ni ruksa kuendelea na masomo.
Vijana na watu wenye jinsia ME aliyeshukiwa au kuhusika kumpa binti mimba akiwa masomoni, moja kwa moja aliwekewa adhabu ya miaka 30 jela.
Je, hawa mabinti wenyewe wanajizuiaje na kuweka juhudi kiasi gani kwa jambo hili, tofauti na kukingiwa kifua na jamii na seeikali juu ya ujauzito kabla ya wakati? Je, wanapotetewa wanateteleka?
Kwa, upande wa jamii na wazazi kwa maoni ya watu tofauti tofauti huko mitandaoni na mitaani, wameamua kunyoosha mikono juu. Wakijisemea " mabinti wenyewe wameshindikana!"
Je, nani alaumiwe sasa? Je, na hao wanaofungwa miaka 30 huko jela nao wajitetee vipi kwa stahili hii?