WIMBI: Ujauzito kwa mabinti wadogo chini ya miaka 18; nani haswa wa kulaumiwa?

I am Groot

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,929
Reaction score
10,747
Nimeona rais Samia akiwa huko ziarani akieleza ni namna gani ameshangazwa na kukuta wamama wazazi (watoto) wodini.

"Nilipokwenda kwenye wodi ya kinamama, na hasa watoto ambao hawajatimia,nimekuta mmoja tu ndio mpevu...lakini wengine wote ni kutoka miaka 15-19, niombe sana, wapeni nafasi watoto wakue kidogo...waacheni waende shule, wapeni nafasi watoto wakue kidogo kuzaa watoto wenzao"Rais Samia

Ni kweli kwa sasa wimbi hili ni kubwa sana na pia ni mzizi wa uwapo wa single mothers wengi hapo mbeleni. Je, ni nani wakulaumiwa? Mabinti wenyewe, wazazi na walezi, Vijana wa rika tofauti huko mitaani, serikali au jamii kwa ujumla?

Ikumbukwe; miaka kadhaa ya nyuma kipindi cha JPM ilitoka amri ya kuwa binti akujifungua akiwa anasoma itakuwa ndio mwisho wa safari yake kielimu. Jambo hili lilipingwa vikali na wanaharakati.

Miaka ya hivi karibuni katika awamu ya sita ya serikali; raisi alitoa tamko kuwa mabinti wakipata ujauzito na kujifungua ni ruksa kuendelea na masomo.

Vijana na watu wenye jinsia ME aliyeshukiwa au kuhusika kumpa binti mimba akiwa masomoni, moja kwa moja aliwekewa adhabu ya miaka 30 jela.

Je, hawa mabinti wenyewe wanajizuiaje na kuweka juhudi kiasi gani kwa jambo hili, tofauti na kukingiwa kifua na jamii na seeikali juu ya ujauzito kabla ya wakati? Je, wanapotetewa wanateteleka?

Kwa, upande wa jamii na wazazi kwa maoni ya watu tofauti tofauti huko mitandaoni na mitaani, wameamua kunyoosha mikono juu. Wakijisemea " mabinti wenyewe wameshindikana!"

Je, nani alaumiwe sasa? Je, na hao wanaofungwa miaka 30 huko jela nao wajitetee vipi kwa stahili hii?

 


Serikali ijenge mabweni kuondoa tamaa ya lifti za Bodaboda Shule ziko mbali watoto wanachoka kwenda kwa miguu na uwezo wa wazazi kuwapa nauli na Hela ya kula hawana
 


Nidhamu katika malezi imetoweka kwa kiasi Kingi.
Wazazi wenyewe wadangaji ujasiri wa kukemea nyendo mbaya hawana.
 
Elimu inabidi itolewe mapema ya kumfanya huyu binti awe anajua athari za mapenzi ya utotoni na ishu za kinga
 
Mimi nahis Usingle Maza Umeharbu Hiki kizazi
 
Mi nadhani kiza hiki cha sasa hv genye zimeongezeka ukali. Vitoto vina mihemko si ya kawaida. Sijui kwa kuwa wanaona matendo ya ngono kirahisi kwenye tv na simu hata sielewi. Ukiwakagua mabegi yao utakuta vitu vya ajabu, maongezi yao ndio balaa zaidi . Wazazi wamefeli kwa 40% lakini 60% ni wasichana wenyewe.
 
Kuna clip moja nmeiona mwanafunzi wa kike under 18
Anakatika,anatingisha kalio linatikisika,show shuleni
Wapo walimu,wanafunzi hapo
Sasa kwa style hyo miuno yake kwann wasimmleeee

Ova
 
Kizaz cha amapiano hiki balaa
Watoto wanaliwa balaa

Ova
 
Serikali ijenge mabweni kuondoa tamaa ya lifti za Bodaboda Shule ziko mbali watoto wanachoka kwenda kwa miguu na uwezo wa wazazi kuwapa nauli na Hela ya kula hawana
Hiyo sio sabab ya mimba mm mkuu Kwan wa kiume ndo hawachoki ungejua mabweni ndo yanaongeza hizo mimba
 
Hiyo sio sabab ya mimba mm mkuu Kwan wa kiume ndo hawachoki ungejua mabweni ndo yanaongeza hizo mimba

Wakiume wengi wanakatiza na kuacha kuendelea na masomo.
Ukosefu wa mabweni ni tatizo kubwa sana lenye madhara yakiwemo hayo.
 
Wazazi wanatakiwa wafanye nini? Toa ushauri sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…