Kuna nyimbo za Verkys zilizovuma miaka ya sabini:
- Mfueni
- Baluti
- Momi Afinda
- Ifantu
- Nakoma juste
- Mikolo Mileki Mingi,
etc
Halafu kuna zile na Salim Abdalah za miaka ya sitini:
- Wanawake Tanzania
- E mola wangu
etc,
Kiboko zadi ni zile za Mbaraka Mwinshehe za wakati akiwa Morogoro Jazz:
- Kulala na Njaa
- Expo 70
- Kwa heri rafiki mpendwa
- Mwenye dada hakosi Shemeji
- Moto wako washa nje
- FAT na Timu ya Taifa 1972
- Tunawakumbuka Wahenga wa Morogoro
- Morogoro Bingwa wa Taifa
Halafu Mbaraka huyo huyo akaja nikosha zaidi alipohamia super volcano kwa nyimbo za:
- Shida
- Nitoe nikawaone wana masika
- Picnic ya Volcano
- Safari Tumerudi salama
Vile vile kulikuwa na Juma Kilaza na wana ambiance aliyemwaga lazi kwa nyimbo za:
- Tunda,
- Wana Ambiance,
- Mwana,
Sikuwasahau watu wa mipasho kama Juma Balo kwa nyimbo zake kama
na Shakila naye mipashoa kabambe kama vile
- Bunduki isiyokuwa na risasi
Ila Tabora Jazz (Wazee wa Kazi) walitia fola sana kwa nyimbo zao kama vile
- Dada Asha
- ooh Mariamu
- Serafina
na wadogo wao nyanyembe Jazz (Vijana wa Kazz) nao wakatoa
- rangi ya chungwa
- wamuonea bure
Balisidya wa Afro 70 (Afrosa) naye alikosha sana kwa nyimbo zake nyingi sana hasa ule wa
Jamhuri Jazz ya Tanga (Wanyama Wakali) nao walitoa burudani sana kwa nyimbo mbalimbali kama vile
- Mganga
- Wanyama wakali
- Fadhili i wapi
Sensera ya Mara Jazz (Sensera) nayo ilikosha moyo wangu kwa vibao kama
Nadhani Western Jazz (Saboso) walikosha zaidi kwa nyimbo zao za
- nachungulia dirishani,
- Rosa (mapenzi yetu yamekuwa ni hasara)
Nyimbo nyingine ni zile za Marijani akiwa Safari Trippers (Sokomoko)
- Georgina
- Tucheze Sokomoko
- Mnaleta Sokomoko
Vile vile namkumbuka Hemedi Maneti alipoanza na Vijana jazz ikiwa bado inaitwa Kokakoka:
Kuna nyimbo nyingi sana ninaweza kukumbuka zilizoachwa na magwiji wa wakati huo kama Atomic Jazz ya Tanga, Kurugenzi ya Arusha,Super Revolution ya Mwanza (majini wa Ziwa), Dar es Salaam Jazz (majini wa Bahari), Njohore Jazz ya Kilosa, na nyingizeo nyingi tu.