Ni kawaida msanii akipata mafanikio makubwa kwa kazi yake ya kwanza kupata tatizo ya kurudia mafanikio.
Hii si kwenye muziki tu. Ernest Hemingway alishawahi kusema kwamba nishani ya Nobel inaharibu uwezo wa muandishi kuandika. Kila akitaka kuandika baada ya nishani anajishtukia "mimi ni muandishi niliyetunukiwa Nobel" anashindwa kuwa huru.
Pia, kutunga mashairi mazuri si sawa na kukubalika, na kukubalika si kutunga mashairi mazuri.
Inawezekana kabisa uzuri wa mashairi (depth, complexity, density etc) ukafanya watu washindwe kufuatikia vizuri msanii akawa underrated (Fid Q) na mtunzi wa mashairi yaliyo overly simple na catchy akakubalika (Darasa).
Kwa hiyo kwetu sisi wengine tunaoangalia depth Darasa hata huo wimbo wake wa kwanza ulikuwa ni bubble gum hip hop at best.
Kuna watoto kibao wanavunja rhymes lakini hawasikiki.