Wimbo mpya wa Darassa CMG umedhihirisha kuwa ile ngoma ya Muziki alibahatisha

Wimbo mpya wa Darassa CMG umedhihirisha kuwa ile ngoma ya Muziki alibahatisha

Wimbo mpya wa darassa 'Hasara Roho'

  • Ni mzuri Sana

    Votes: 15 40.5%
  • Ni mzuri kiasi

    Votes: 5 13.5%
  • Wa kawaida tu

    Votes: 13 35.1%
  • Ni mbaya

    Votes: 4 10.8%

  • Total voters
    37
Usitake kuikatisha hazina yetu tamaa....kwasasa nani kama darasa...Ngoja watu wamalize msibe waje hapa naona unataka kutuletea balaa
 
Tukiacha unafiki mashairi ya hiyo nyimbo ni Kali sana,Video Kali sana...Beat ndo imemwngusha kwa kiasi flan
 
Wimbo mzuri kwa upande wangu though nimechelewa kuuelewa, Leo ndio umeanza kuniingia kumoyo, siku wanautambulisha nilishindwa kuujaji
 
yani muziki/toomuch na huu mpya inafanana kila kitu
yani sio mbunifu hata kidogo aaaghrr
bora nyimbo zake za zamani za heya heya
 
Tusiwe wanafiki ukweli wimbo wa kawaida sanaaaaaa tena sanaaaaaa
 
Nasikia kuna wasanii walichinja kondoo ili Darasa asitoe hit nyingine...za kunyapia nyapia
 
Naona team hapa ndo zinashambulia haziamini jamaa ndo ana take over
 
Tatizo la mashabiki wa Tanzania eti ili uonekane umefanya ngoma Kali basi lazima ufanye kollabo na wasanii wakinaijeria
 
Ni kawaida msanii akipata mafanikio makubwa kwa kazi yake ya kwanza kupata tatizo ya kurudia mafanikio.

Hii si kwenye muziki tu. Ernest Hemingway alishawahi kusema kwamba nishani ya Nobel inaharibu uwezo wa muandishi kuandika. Kila akitaka kuandika baada ya nishani anajishtukia "mimi ni muandishi niliyetunukiwa Nobel" anashindwa kuwa huru.

Pia, kutunga mashairi mazuri si sawa na kukubalika, na kukubalika si kutunga mashairi mazuri.

Inawezekana kabisa uzuri wa mashairi (depth, complexity, density etc) ukafanya watu washindwe kufuatikia vizuri msanii akawa underrated (Fid Q) na mtunzi wa mashairi yaliyo overly simple na catchy akakubalika (Darasa).

Kwa hiyo kwetu sisi wengine tunaoangalia depth Darasa hata huo wimbo wake wa kwanza ulikuwa ni bubble gum hip hop at best.

Kuna watoto kibao wanavunja rhymes lakini hawasikiki.
 
Malengo, Kama utanipenda, Too much, Muziki na sasa Hasara Roho sijataja za zamani halafu useme anabahatisha!
 
Wimbo mzuri ila haufikii Muziki.

Angesubiri subiri kwanza....people will find no significance difference between two
 
Back
Top Bottom