Wimbo mpya wa Darassa CMG umedhihirisha kuwa ile ngoma ya Muziki alibahatisha

Wimbo mpya wa Darassa CMG umedhihirisha kuwa ile ngoma ya Muziki alibahatisha

Wimbo mpya wa darassa 'Hasara Roho'

  • Ni mzuri Sana

    Votes: 15 40.5%
  • Ni mzuri kiasi

    Votes: 5 13.5%
  • Wa kawaida tu

    Votes: 13 35.1%
  • Ni mbaya

    Votes: 4 10.8%

  • Total voters
    37
Huyu jamaa kaanzisha thread zaidi ya hii leo zote za kumponda darasa wivu
 
We jamaa una masihara mpaka basi.

Subirini bodaboda waipatee

Darasa HASARA ROHOv/s Yang dee BONGO BAHATI MBAYA.!!!!!!!???


Okkyyy wacha mawazo ya kila mtu yaheshimiwe.
Ss bodaboda unaweza kumtumia kuona kuwa huo ni wimbo bora
 
Yaani bonge la ngoma halafu we jamaa unasema mara ya kwanza alibahatisha?! Though rhythm kimtindo imefanana na Muziki but still kwenye hii ya sasa kuna vitu vipya vya kutosha!! Na Big Up kwa producers vile vile manake chemistry iliyofanywa kwenye beats, ni ya kiwango cha juu!!
Karagabahu
 
Nimetoka kusikiliza wimbo wa Yang Dee hapa.

Kwa wanao fananisha ngoma ya DEE na DARASA.


Bila shaka yoyote anayeupa point wimbo wa DEE hakika age zao lazima zitakuwa zinaendana yeye na D.



Msikilizeni tena na tena na tena Darasa mtaelewa kuwa hajatuangusha.
 
Ipe muda ikae masikioni mwako, we mwenyewe utaanza kuiimba hata ukiwa church
 
Ss bodaboda unaweza kumtumia kuona kuwa huo ni wimbo bora
Hah hah hah mkuu kautafiti kangu upande ninaoishi nimegundua watu wanakalili kwa haraka nyimbo kupitia bodaboda kuliko kusikiliza katika radio muda huo hawana.


Kijiwe cha hapa nilipo wimbo ukitoka tuu hauupendi unaupenda utaukalili tu.

Ukipanda boda unao ukishuka unao.

Binafsi sikumbuki lini niliangalia Tv au Radio mkuu.
 


acheni wivu wa kike...mashairi makali...wimbo mkali...production ya audio kali...ya video nayo ndo usiseme....wasanii wachache sana wanaandika mashairi yanayobebeka kichwani kirahisi kama huyu....huuu utakua wimbo mkubwa ipe muda...wabongo wengi ni fuata upepo we tulia utaona.

Jamaa ni mwimbaji mzur Tangu kitambo, japo naweza kusema hakuwa na bahat ya kung'ara. Ndio maana wengi wanadhani kaanza na Darasa... kumbe yumo kitambo..
Wimbo huu Video nzur lkn bado jamaa hakuwa na jipya humu... kitu kizuri hakisubiri upepo, kizur kizur tu hata watu wasipokipokea lkn kinabaki kuwa kizuri...
 
Ni mapema mno kusema kuwa huu wimbo ni m'baya au ni mzuri,ngoja tuipe muda ndio tutajua ukweli.
Tukiupa muda maneno yatabadilika, kuongezeka, ama kupungua? ?? Au tusubir remix! Huu ndio huuhuu hata tukisubir
 
Nyimbo za darasa sio za kukurupuka na kusema et kabahatisha. Hii ngoma ni kali na ww ipe muda uta realise kuwa ulikosea ku judge hii ngoma mapema. Ngoma kali ww hiii acha chuki [HASHTAG]#Hasara[/HASHTAG] Roho Pesa Makaratasi [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Wewe kachambua mchele. Kuchambua mziki ni kazi. Ngoma kubwa sana hii mpya tena kuliko maisha na muziki. Alafu mlishakalili miziki inayofanana
 
Wewe kachambua mchele. Kuchambua mziki ni kazi. Ngoma kubwa sana hii mpya tena kuliko maisha na muziki. Alafu mlishakalili miziki inayofanana
e9baad6c9641be1b1d73ee8887603702.jpg
 
Swali la msingi umeanza kumfahamu au kusikiliza ngoma za Darasa kuanzia lini? Hiyo muziki mmekuja kuijua ninyi sasa lakini Darasa yuko vizuri kitambo!wewe kuna siku utakuja kusema Jay mo proffesor Jay Mwana FA na watu wa kariba hoyo wanabahatisha!
acha porojo, single iliyomtambulisha ilikuwa muziki, hatukuwa tunamjua labda nyie wa kitaani kwake
 
Beat safi, kinanda kimenogesha wimbo na mistari ya 2017...Ujanja wa nyani mjini utaingia kingi,
Meli inaelea feli,inazama shilingi...dunia iweke tuzo ya wachukiaji
 
Darassa kaamua hiyo ndo iwe style yake ya kurap hapo mi sioni tatizo mleta uzi endelea kusikiliza nyimbo za wabana pua hizi tuachie sisi.
 
Back
Top Bottom