Wimbo mpya wa Mrisho mpoto-chocheeni kuni

mojoki

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
1,313
Reaction score
290
Najaribu kujiuliza hii nyimbo Mpoto anaongelea Malumbano ya kidini yaliyojitokeza hivi juzi kati, au nyie mmeelewaje wadau: Sehemu ya Mashairi ni pale anasema

"Waliopo hatuwataki, wanaotaka tuwape hatuwaamini
(Hapa nadhan anaongelea CCM na Chadema)

Hapa nadhan ni dongo la wale madogo hali iliyopelekea mmoja kukojolea msahafu...

Maneno siku zote yanauma na yanachefua ukielewa maana yake.
Kwa mfano neno la kitoto kumwambia mtoto tunasema watoto wanacheza
Neno la kitoto kumwambia mkubwa tunasema mtoto anakua
Mtoto akisema baba ile ndege yangu, baba hata kama hana biskeli umwambia ikitua ntakuletea. Lakini maneno ya kitoto mtu mzima kumwambia mtu mzima kunawalakini"...

Kiitikio cha Nyimbo kinasema


Chocheeni kuni moto uwake ugali uive mnachotaka kitokee
Halikeni mamruki, wakija wangojee, mikeka wawekee
Wanachotaka kitokee
Chochea X 8
 
Hana jipya kafulia tayari mkenya uyu.
 
hana tofauti na mafisadi, sio mtanzania huyu labda alikua anawaimbia wakenya.!
 
kwani amebadili uraiwa wakuu mbona mnasema ni mkenya!!???
 
Ni mndendeule wa wilaya ya Namtumbo kijiji cha mchomoro pande za songea huko..huo ukikuyu kautoa wapi?

Mkuu JF siku hizi wapotishaji wengi mtu anasema anachojisikia hata kama hakina ukweli wowote.
 
Mkuu JF siku hizi wapotishaji wengi mtu anasema anachojisikia hata kama hakina ukweli wowote.

Wajanja tushamuelewa kwanini jamaa kamuita mkenya kasoro nyie tu kalagabaho
 
mtamtupia sana madongo mjomba na wimbo wake lakini ndo yale yale
ukirusha jiwe ukasikia yalaaa ujue limekupata!
ana falsafa kubwa sana kwenye huu wimbo au shairi alilotoa kipindi hiki!
hauitwi chochea unaitwa narudi nyumbani!

HAKIKA TULIOWAPA WAMETUSALITI NA WANAITAKA ndo hivyo tena HAWAAMINIKI!
 
ni dadavulie best!! mie mmojawapo wa waliochwa na treni ya mwakyembe, lol!

naona uliowaomba msaada wamekuchunia, ngoja nijipendekeze

aliwahi kualikwa na wakenya kwenda kutumbuiza Ulaya lakini akiwakilisha nchi ya kenya.

Lakini ni kwa sababu sie watanzania hatuthamini vya kwetu mie wala sikumlaumu kwa hicho. Maana JK alishakataa hataki kumuona Mpoto kwenye shughuli yake yoyote. Siku ukimuona Mpoto kwenye hafla ambayo JK yupo basi katambikie
 
Sio kuwakilisha kenya tu, pia kwenye hotuba yake alisema Mlima Kilimanjaro upo Kenya.


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 

Ndugu yangu shapa tuna watanzania na serikali ya tanzania,lazima ukumbuke serikali hii kwa miaka mingi imekoma kusimamia maslahi ya watanzania.
WATANZANIA TUNAMTHAMINI MPOTO NA UKITAKA KUJUA KWANINI SERIKALIHAWAMTHAMINI FUATILIA MASHAIRI YAKE!si muda mrefuatitwa mchochezi!
 
Jinai kivipi kwani kauhamisha? Watu wanachukua ziwa mmenyamaza tu ngoja iko siku tutasikia arusha iko kenya.....
njaaa mbayaaa , kuwakilisha Kenya ni sawa labda angefanya kwa njaa zake, lakini kutoa wasaa/hotuba kwamba Kilimanjaro upo Kenya ni kosa la jinai!
 
Jinai kivipi kwani kauhamisha? Watu wanachukua ziwa mmenyamaza tu ngoja iko siku tutasikia arusha iko kenya.....
alisemaga nyerere katika nchi yenye serikali legelege vijambo vingi si ajabu kusikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…