Wimbo "pale kati patamu" wa Ney wa mitego wafungiwa rasmi

Ndo wameupa promo. Hata nlkua siujui, ngoja niutafute..!
 
tatizo huyu jama anaiga swagga za kimarekani kama tyga,lil wayne,yg,young thug buster rhymes hawa wanaimbaga matusi tuuu
 
Usikute wenzio kufungiwa wanaona raha wanapata kick, maana wasanii wetu hawa
 
Hii haina maana.Wimbo ushasambaa mitandaoni

Ilipaswa wamfungie hata miaka miwili asifanye shoo njaa impige ndio atajifunza

Shame on you BASATA
kuweka kumbukumbu sawa,ni haohao basata waliwahi kumfungia shilole kutafanya mziki,lakini baada ya shilole kuwemo katika orodha ya watumbuizaji wa chama tawala wakati wa kampeni zuio lile liliyeyuka kwa namna isivyo eleweka.kutegemea basata kuja na jambo la kifanisi kwenye tasnia ya muziki wetu ni kupoteza wakati bureeeeee
 
Mtani nakuunga mkono nadhani BASATA awajitambui wanafanya nini wao panatakiwa pafumuliwe pale na napendekeza pawekwe watu wapya hao wapumzishwe tu
 
nini ney , ajifunze nyimbo tamu kwa madogo kama Jux aisee wimbo wa Wivu mtamu sana, natamani ndo ungekuwa umeimbwa na diamond
 
wasio weza kuimba ndio wanafanya haya , au wawe uchi au waweka maneno yasio na maadili
 
Aliyeusikiliza Wimbo Naomba Aniwekee Mistari Hapa
 
Huu ni ujinga wa basata

Wanatakiwa wawe na kitengo cha kukusanya nyimbo kabla msanii hajaisambaza lazima ipate baraka za basata kwa kuangalia maudhui yake

Kabla haijaingia kitaa

Tatizo basata imekaa kizeekizee hawana jipya
 
kuishi bongo usenke tu kila kitu wanafungia! wenzetu wanatoa mixtapes na cover vile wanavyotaka hadi raha
 
Kwa maana nyingine wamekuwa watu wa kusikilizia au kuusoma mchezo Kwanza
 
Nakesha kama popo nikitafuta mademu pale kati patamu pesa ni tamu lakini pale kati patamu..
Fungeni tu umekosa maadili
 
Bravo BASATA fungia wahuni wote. tena inatakiwa sio wimbo bali na msanii piga chini for 2-3 years!! ili wawe na discipline.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…