Wimbo "pale kati patamu" wa Ney wa mitego wafungiwa rasmi

Wimbo "pale kati patamu" wa Ney wa mitego wafungiwa rasmi

Sorry to say this but BASATA have some loads of stupidity if not negligence on them
Hiki kitengo ndio kilitakiwa kiratibu kazi zote za wasanii kabla hazijazalishwa! Uwezo huo upo sasa inakuwaje wanasuburi kazi itoke isambae kwenye jamii ilete madhara ndio wao waje na blah blah za kuifungia? Huku si kutengeneza mazingira ya rushwa?
Sorry again to say this but I can sniff some stupidity on them

Maoni mazuri lakini kamwe siungi mkono suala la kusema kazi zikaguliwe na Basata au yeyote kabla....kutatokea uminywaji mkubwa wa ubunifu na uhuru wa kujieleza....mwishowe wataelekezwa mpaka ni nini cha kuimba.

Tuna ombwe kubwa la kiutendaji kwa maofisa wetu, mkithubutu kuwapa kila rungu wataishia kufanya wanachojisikia kwa utashi binafsi....kuna mengi ya msingi tunatarajia kutoka kwa hivi vyombo na wamestuck.

Kwa mfano leo hii uwape Polisi wetu hawa meno ya kudhibiti kila asiyevaa sawasawa akamatwe basi hata Wamasai watakoma....au trafiki akikukamata na akataka tu lazima uwe na kosa ujue huchomoki.

La msingi ni hao hao Basata wawe wanakutana na Wadau mara kwa mara na kuwafanya wao kwa wao kusimamiana na hata kupeana adhabu pale wanapokiuka...kwa mfano Producer, video directors, Mameneja wa Wasanii, Presenters wakiwagomea Wasanii wanaokiuka maadili Msanii atakwama tu.

Kwani hizi Redio na TV zinadhibitiwa na nani kwamba kabla hawajaenda hewani wakaguliwe na chombo cha serikali...lakini kwa kuwa wanajua wakikiuka watakutana na rungu huko mbele wao wenyewe wanajidhibiti.

Chonde chonde mwendawazimu si wa kupewa rungu.
 
Hata mimi nimefkiria hivyo mkuu kwann nyimbo ya msanii yoyote hapa bongo isipite kwanza kwao waipitie kisha ndo iruhusiwe kwenye ma blog n vituo vngne vya burudan....Yaan unafungia kwenye Redio wakati watu kwenye simu zao ipo
Hapana kaka....Wasanii na wadau wao wasimamiane wenyewe....sio wagonjwa wa aikili hao.
 
mngempiga BAN yeye mwenyewe ,jamaa huwa simfagilii kabisa kwa style yake ya nyimbo zake,hazina adabu anadhalilisha sana wanawake hana heshima nao kabisa utadhani yeye katoka juu hajazaliwa na mwanamke shenzy kabisa huyu jamaa
 
sjaona maana ya kuufungia huo wimbo while is already spreaded
 
TCRA na BASATA wote wanafiki Kuna kipindi nyota ndogo ft nonini, kwenye verse ya nonini akatukana (mse****) ilipigwa sana kipindi kirefu baadaye wakaanza kuimute, sasa njoo kwa hawa wanafiki TCRA, jana saa nne cloudstv walikuwa na kipindi cha NEW DROP Kuna nyimbo ya Snoop dog ft Jeremiah, hiyo video ilikuwa na stripper wamevaa chupi cha kamba alafu wezele la hatari wameshikiliwa mlingoti twerking za hatari yaani hata chura ya snura inasubiri. TCRA na BASATA ni sawa na yule anayeichukia nyama mbuzi lakini mchuzi wake wanakunywa, alafu nimegundua ukitukana kwa kiswahili kwao tusi ila kwa kingereza sio tusi. Kuna nyimbo kibao za kingereza watu full kutukana na ukizingatia siku hizi English medium kibao wanatuharibia watoto wetu, sasa sijajua hizi nazo BASATA hawazioni au labda ngeli hazipandi.
 
BASATA wakati nyumba ya sanaa inavunjwa walikuwa wapi? Hawa wanaafiki sijui wanasimamia sanaa gani? Kwanini wakiokoe chuo cha sanaa Bagamoyo kinaelekea kubaya sasa? Au kazi yao ni kufungia nyimbo za Bongo Fleva tu?
 
Pale Kati Patamu,patamu tamu!
Ata Jf ni Tamu,ila Pale Kati Utamu Wake ni Adimu!
 
Huyu jamaa ana kera sana na amepitiliza sana muziki umemshinda kabisa!
Kaka mkubwa, huyu kuna ile BIASHARA isio rafiki kwa jamii, anafanya. Huku ktk music kaja kujificha tu kama chaka lake!
 
Kabla ya BASATA sisi kama jamii tulikua tuna nafasi ya kuzikataa nyimbo za aina hii ila kwa unafiki wetu tuna download na ku-request kila siku kweye radio station na kwa nini media house wanaruhusu nyimbo chafu kuchezwa wakiwa wanajua kua ni chafu yaani mpaka BASATA watoe tamko ndio wao wanavunga huu ni unafiki uliopitiliza kuna sehemu ya jamii tena kubwa ni mashabiki wa hizi nyimbo ndio maana zinapata air time naamini ukienda mkito na yotube utakuta idadi ya kubwa ya watu wameupakua tayari.

BASATA wana nafasi yao ila sisi kama jamii tuna nafasi kubwa kama kunatokea moral decay hakika athari zake zitatukuta sisi sio BASATA binafsi siwezi kuwalaumu BASATA maana tumeshuhudia tokea anaanza kuutangaza huu wimbo na picha zake tukakaa kimya na mwenyewe alisema kua itafungiwa,CB mpaka leo kuna nchi harusiwi kufanya matamasha kisa domestic violence na mashabiki hawako tayari kumpokea ingawa tukio limetokea muda mrefu.
 
Baraza la sanaa BASATA limeufungia rasmi wimbo wa ney wa mitego wa pale kati patam
Leo.16july
 
Pale Kati Patamu,patamu tamu!
Ata Jf ni Tamu,ila Pale Kati Utamu Wake ni Adimu!
Nimejaribu kuusikiliza huu wimbo kwa mara kadhaa bado sipati sababu kamili ni kwa nini mnamshukia Nay kiasi hiki.

Kwa wimbo ule wa 'shika adabu yako' naunga mkono hoja kwani kuna maneno alitamka moja kwa moja..lakini kwenye wimbo huu sioni mahali ametumia tusi la moja kwa moja.

Labda kama anaadhibiwa kwa zile picha alizoziambatisha....hapo naunga mkono.

Hivi tukiwaweka mezani Nay 'pale kati patamu' na Ya moto 'una rambo mimi nina muwa' na wote wakajitetea kuwa hawana maana hiyooo...ni kwamba tutamuhukumu Nay na kuwaacha Ya moto?.

Au wimbo wenye maneno 'napenda unavyokata na kunipa taratibu' una tofauti gani na Nay anaposema 'navutiwa na wote zikinipanda mimi nabeba yoyote'..

Siungi mkono ukiukwaji wa maadili lakini napata picha kama vile afanye mwingine lakini sio Nay.
 
Nimejaribu kuusikiliza huu wimbo kwa mara kadhaa bado sipati sababu kamili ni kwa nini mnamshukia Nay kiasi hiki.

Kwa wimbo ule wa 'shika adabu yako' naunga mkono hoja kwani kuna maneno alitamka moja kwa moja..lakini kwenye wimbo huu sioni mahali ametumia tusi la moja kwa moja.

Labda kama anaadhibiwa kwa zile picha alizoziambatisha....hapo naunga mkono.

Hivi tukiwaweka mezani Nay 'pale kati patamu' na Ya moto 'una rambo mimi nina muwa' na wote wakajitetea kuwa hawana maana hiyooo...ni kwamba tutamuhukumu Nay na kuwaacha Ya moto?.

Au wimbo wenye maneno 'napenda unavyokata na kunipa taratibu' una tofauti gani na Nay anaposema 'navutiwa na wote zikinipanda mimi nabeba yoyote'..

Siungi mkono ukiukwaji wa maadili lakini napata picha kama vile afanye mwingine lakini sio Nay.
Nina uhakika wengi wamemhukumu pasipo hata kuona wala kusikiliza mashairi ya wimbo husika.
 
Back
Top Bottom