Hapana mkuu sio roho mbaya ni maudhui ya wimbo wenyewe na muda uliobaki. Ukitoa leo zimebaki siku 42 tu kabla wenye inchi hawajaenda kuchagua viongozi wao. Albamu tutanunua tuuu. Isitoshe mpaka albamu ikamilike inachukua zaidi ya miezi minne yaani apate vijinyimbo vingine vya kujazilizia, hii nayo inachukua muda. Wimbo mmoja kutuwekea hapa sio ishu sana kwa sababu baada ya Oktoba 31 thamani yake itashuka hadi 13% au pungufu. Kuna maana gani kuficha habari inayotakiwa sasa kwa minajili ya kuuza baadae? Kwanza atapunguza gharama za uzinduzi wa albamu kwa sababu utakuwa umesha jizindua wenyewe kitakachofuata ni mauzo mfululizoooo!!!!
Kwa maoni yangu mwenye no auweke hapa wananchi tujisikilizisheeee!!!!!!