Wimbo wa Harmonize wa Sandakalawe wazuiwa youtube, sababu wasema ni kuiuka hakimiliki za kampuni ya EMPIRE

Wimbo wa Harmonize wa Sandakalawe wazuiwa youtube, sababu wasema ni kuiuka hakimiliki za kampuni ya EMPIRE

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535
Harmonize.png

Wimbo wa msanii nguli wa bongo flava Harmonize unaoitwa sandakalawe, umezuiwa youtube kutokana na kile kinachosemwa kuwa ni kukiuka hakimiliki za kampuni ya usambazaji mziki ya EMPIRE. Mpaka sasa haijajulikana ni kipengele kipi cha hakimiliki kilichokiukwa lakini tetesi zinasema ni shutuma za wizi wa wimbo ambao unasambazwa na kampuni ya EMPIRE.

Hii si mara ya kwanza kwa Harmonize kukumbwa na matatizo ya hakimiliki dhidi ya wasanii wengine, wimbo wake wa "Your Body" unaofanana na wimbo wa Papa Wemba wa "show me the way" alioshirikiana na Burna Boy kutoka nchini Nigeria uliondolewa kwenye album yake ya Afro East kutokana na matatizo ya haki miliki.

Pia amewahi kukwazana na wasanii mbali mbali kama Magix Enga kutoka Kenya, Rosa Ree kutoka Tanzania na wasanii chipukizi Lizu Dady na Phamo S kwa shutuma zinazofanana za kutumia nyimbo zao bila ya maelewano.

Mpaka sasa msanii huyo hajatoa neno lolote baada ya hit song hiyo kufungiwa kwenye mtandao wa youtube.
 
Sijui tunaelekea wapi! Wanaojua hata hatuwapi time Ila hawa wenye maneno mawili nyimbo nzima ndio tunawapa time

Nyimbo mbaya, kuipenda mpaka uambiwe iskilize kwenye mziki mkubwa ama utaskia video ndio kali

Si konde wala kaka yake Simba now ni hovyo sana
 
Mateam ndo yameua msanii sasahiv ili utoke ni lazima uwe kwenye team 3 (wcb,king,konde)

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Mmakonde ameishiwa...ni bangi ana vuta au ni nini?.

Kipaji anacho ila kila siku ni products mbovu tu.
 
Frankly speaking..hizi ndo ngoma kali kwangu kwa sasa

✓Mapenzi ya Rich Mavoko.

✓Temptation ya Brian Simba.

✓Najiweka ya Jay Melody.

Ila muziki umehodhiwa na watu ambao hata nyimbo takataka nazo zinalazimishwa kuwa hitsongs.
 
Back
Top Bottom