Wimbo wa Iddi Amin Dada

Sasa tunawakumbuka
Walio kufa kwa tabu
Bila hata matibabu
Wengi hawana hesabu
Walio kufa kwa tabu duniani
Mwana Lumumba wa kongo
Alimpiga vigongo
Wakamvunja mgongo
Wakamtoa ubongo
Wala sisemi uongo
Ni ukweli
Tom mboya wa Kenya
Si kiongozi mbaya
Kala risasi ya taya
Maharamia wabaya
Wala hawaoni haya kumuua
Na maiti na maiti si mwingine ni amini
Wananchi ndugu zangu mwasikia
Maneno yaliyo semwa majuzi huko Uganda
Maiti nazo husema aaaa
Wacha Tanzania utaitambua.
Amini kapiga ngoma gaddafi kaimba wimbo
Maiti nazo husema aaa wacha tanzania utaitambua
Gaddafi wewe Tanzanian utaitambua
Amini wewe Tanzanian utaitambua
 
Mwaka Gani ilikua mkiimba nyimbo hizi!??
 
Kitengo cha propaganda kilikuwa na nguvu sana wakati wa mwalimu, nakumbuka shule tulimuimba sana kambona na chipaka. Kuwa kambona alimwambia chipaka pindueni mkiweza nitawapeni mapesa nikirudi safarini wingereza.
 
Nakumbuka mchamcha shule ya msingi miaka ya ya 80
 
Nasimama nasimama mliMa kasetii, naionaa naioNa kongo zaireee,
Elizabeth eliza mamaa wayoowayoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…