Wimbo wa kiswahili uliotrendi sana mitandaoni uliotengenezwa kwa AI

Bawabu wa pili

Senior Member
Joined
Nov 14, 2025
Posts
147
Reaction score
433
Watu wengi wamekua wakiuskiliza huu na umewahudumia sana lakini bila kujua ukweli ya kuwa huu wimbo umetengenezwa kwa AI. Ukiangalia kuanzia mpangilio wa sauti, mguso wa hisia na namna ulivyokaa kugusa mioyo ya watu huwezia amini kuwa hii ni AI, namna ulivyopangiliwa unazidi hata ubunifu na wa wasanii wengi tuu.

Tuseme nini sasa? wasanii wetu wapo katika hali mbaya kwasababu ya AI kushika hatamu hadi kwenye mziki na kuufanya wimbo ukaenda viral kuliko hata nyimbo za wasanii wenyewe.

Ulivyouskia kwa mara ya kwanza ulidhani imeimba kwaya gani? na je ulijaribu hata kuwaza kuwa AI ina weza kufika hatua hii ya kufanya mambo kwa level za juu kuzidi hata binadamu?



Your browser is not able to display this video.

Huu wimbo una mwezi mmoja tu lakini una zaidi ya viewers 800,000 youtube na umewaponya sana watu wengi sana lakini kuanzia sauti (audio) hadi video yake ukiitazama kwa makini ni AI.

​
 
Nilikuwa najiuliza nani kaimba wimbo mzuri hivi
 
Kuna ule wa no reform no election... Ule ndo balaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…