Wimbo wa Papii Kocha umenitoa machozi

mapessa

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
664
Reaction score
1,168
Daaah huyu jamaa niliwahi kusema akirudi kuimba Tena Dunia itasimama.

Yasome mashairi yake hapa.

Verse 1.

Dunia inazama, naangalia,
Sina cha kufanya,moyoni naumia.
Mawazo yangu oh, naangamia
Uko wapi Mungu wangu we,hunioni nalia

*Kumbe ulikua unanisikia , unaniangalia.....weweeee
Likapotea,tumaini langu ila imani ikaingiaa....×2

Chorus

Waambie, uliniona,nilipokuomba uliskia,na ukaitika.
Mungu wambie,uliposema uwaja, wala hukukosea njia, na ulifika.
Mungu wambieee, niwewew tuuu, niwewee tuuu, wuwuwu.
Mungu wambie eeh, niwewe tuu uliesababisha leo imefika.

Verse 2.
Wambie, kila siku ni zawadi, hakuna heshima inayozidi uhai.
Ni Nineema na Rehema, wawe ha hekima unazitimiza ahadi,
Ooh ooh wambie, hawapaswi kukata tamaa, sababu daima haupo mbali.
Ukipotea mwanga, gizani ndo nyota hunga'aa mwanga mkali.

Wambie,
Wasiache tumaini ndo imaniiii iii
Wasiache kukuamini ndo amanii ii iii

Chorus

Waambie, uliniona,nilipokuomba uliskia,na ukaitika.
Mungu wambie,uliposema uwaja, wala hukukosea njia, na ulifika.
Mungu wambieee, niwewew tuuu, niwewee tuuu, wuwuwu.
Mungu wambie eeh, niwewe tuu uliesababisha leo imefika. ×2

Link hii kuitazama video yake
 
Nyimbo nzuri lakini hakuna sehemu inayosababisha mtu kulia labda kama una husianisha maisha yako na nyimbo au una hisia binafsi.
 
[emoji28] Ngoja labda nijaribu kuvuta hisia za kifo cha hayati baba wa taifa naweza nikalia [emoji24][emoji24]
 
Mleta mada inaonekana una hisia za karibu sana!.. Hebu tafuta na hii nyimbo Billie Holiday - Gloomy sunday nasikia wasikilizaji wengi wamejiua baada ya kuisikiliza!..[emoji6]
 
Wabongo watakuambia kesi yao ilikua ni Kiki ya huo Wimbo. [emoji23] [emoji23]
 
Mleta mada inaonekana una hisia za karibu sana!.. Hebu tafuta na hii nyimbo Billie Holiday - Gloomy sunday nasikia wasikilizaji wengi wamejiua baada ya kuisikiliza!..[emoji6]

kwa hiyo we unamshauri asikilize huu wa Billie ajiue kabisa sio? hahaha JF never boring
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…