Msitoane macho......someni katiba....
2.-(1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la
Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni
pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania
inapakana nayo.
(2) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali
ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Rais aweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika
mikoa, wilaya na maeneo mengineyo, kwa kufuata utaratibu
uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na
Bunge: Isipokuwa kwamba Rais atashauriana kwanza na Rais
wa Zanzibar kabla ya kuigawa Tanzania Zanzibar katika
Mikoa, Wilaya au maeneo mengineyo.