Ndio Pita huku ni jina la wimbo mpya wa Dulla Makabila, Makabila kama msanii katumia kipaji chake kuwasilisha mawazo/ujumbe wake kisanii kwa jamiii.
Alichoimba Dulla ni uhalisia wa matukio yanatokea kwenye jamii zetu kila siku,tulitegemea tupate ujumbe kama wa dulla kutoka kwenye vikundi vya kuimba nyimbo za Dini lakin tumepata kutoka kwa msanii wa Singeli ndio hakuna tabu.
Kama nakumbuka mwl wa Kiswahili alinijuza kazi za Fasihi kwa pamoja yani fahisi andishi na simulizi pamoja na sanaa ambao ni ufundi wa kuwasilisha mawazo ya mtunzi ni
Kuelimisha, kuburudisha, kufikisha jumbe mbalimbali, kuonya, kukemea...nk
Dullla kasimamia vyote hivyo zaidi ya kusikiliza midundu tu pia tusikilize Ujumbe, katukumbusha nyakati za mwisho zipo na kila mtu atatoa hesabu zake.
Tukumbuke ukiwa hai Bwana Yesu anasimama kama wakili ila ukifa anasimama kama Hakimu.
Tubadilike, ndio pita huku